RPC Lindi Watanzania wanaomba tamko lako, uhujumu uchumi waendelea huko Lindi

kimbendengu

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
6,716
Reaction score
12,116
Jamani tunaomba muendelezo wa Yale matamko ya uhujumu uchumi yaendelee huko Lindi leo wafanyakazi wa Azam media walishindwa kufanyakazi na kuchelewa safari yao kutokana na barabara ya wilaya ya Ruangwa kuwa na makorongo, tope, sasa naomba wale makamanda wa matamko mkuje huku haraka video hii kwa ushahidi
Your browser is not able to display this video.
 
Haa
Mwaka Wa Tabu Ni Tabu Tu
Huu Mwezi Leo Ni Tarehe 20.02.2020 Mbili Mbili Tele, Sifuri Nazo Tele 😅😄😃😂😁

Yaani Jaji, Bashiru, Leo Tena Azam
😏😐🤔😶😑🤨
 
Inchi inaongozwa kipumbavu kweli. Hadi kuonesha ubovu wa miundo mbinu ni uhujumu uchumi?
 
Halafu inashangaza kusikia mkubwa mmoja, badala ya kupongeza wazalendo wa aina hiyo waliofichua hali mbaya kiasi hicho cha barabara, badala yake "anaropoka" kuwa eti wanaopiga picha za aina hiyo na kuzirusha mitandaoni, wasakwe na wakipatikana watafunguliwa kesi za kuhujumu uchumi!
 
Naona juhudi kubwa ukarabati miundombinu Hifadhi ya Ngorongoro, hadi wameomba jeshi lisaidie kwa dharula baadhi maeneo.Nguvu ya media ni kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado tunajisifu tumenunua mandege makubwa sana tena kwa keeeshiiii
Naona juhudi kubwa ukarabati miundombinu Hifadhi ya Ngorongoro, hadi wameomba jeshi lisaidie kwa dharula baadhi maeneo.Nguvu ya media ni kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Safari ya wafanyakazi wa Azam Media waliokuwa wakielekea Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kwa ajili ya kurusha matangazo ya mechi ya VPL kati ya wenyeji Namungo vs Azam FC ilisimama kwa muda kutokana na kuharibika kwa barabara ya kutoka Nanganga kwenda Halmashauri ya Ruangwa.

In God we Trust
 
Nadhani sisi tuna angalia kwa upande wetu na wao wana angalia kwa upande wao,laiti soote tungeangalia upande mmoja,sasa hivi ie 2020 tungekuwa mbali tena mbali sana.

Tuekekeze mikono yetu juu kumuomba ALLAH atujaalie tuwe wamoja na tutofautiane kina mawazo kwa lengo la kujenga na siyo kubomoa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Mkishamaliza kufurikafurika huko mje tuwapige bei kwenye viazi, mihogo na mahindi".-mwisho wa kunukuu
 
Kwani anaye bomoa ni yupi mkuu?
In God we Trust
 
Inawezekana alipitiwa tu
In God we Trust
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…