RPC Mstaafu Rwambo: Ni Haki ya Mwananchi kujua kwanini anakamatwa na Polisi ni lazima ajieleze anatokea Kituo gani

Namjua Rwambo tangu akiwa OCID Njombe hadi RPC Oyster bay ni Jamaa mmoja Safi sana πŸ˜‚

Ungekuwa wa hapa Mjini ungelijua kipindi chake Cha Michezo na akina Kipenka na Mzee wa Bao Likwepa wa Kariakoo πŸ˜„πŸ˜„
Mie mjini kitambo
 
Nadhani tuanze kujilinda wenyewe,kama unahisi unafatiliwa UMUGHAKA tafuta bisibisi yako au kisu kizuri kaa nacho kiunoni,mtu akija haeleweki eti anataka kukuhoji bora mmalizane mapema kuliko kwenda kukumaliza huko
Bahati nzuri au mbaya ni kwamba,hao wanawake nilishawapa Taarifa mapema sana!
Mimi nawasubiri tu ili waone utofauti wa kumkamata mwanaume UMUGHAKA na hao wanawake waliozoea kuwakamata!,siku hiyo ndiyo watajua kutofautisha kati ya kumkamata mwanaume na mwanamke!
Siku hiyo ndiyo watajua kumbe nchini hii bado inawanaume!
 
Ndio shida yetu watanzania mada kama hizi za elimu ya jamii kuhusu haki raia kwenye ukamataji. Hatutaki kuchangia na kujifunza si ajabu wangeingia ma-afande wa JF na ku-extend statement ya boss wao kwa kina zaidi upate somo la bure siku ukikakatwa hasa kwenye kadamnasi ujue cha kufanya.

Ngoja sasa waambiwe kuna vocha za bure za tsh 1000 au story za uchawi lisaa limoja utakuta mada Ina views 10,000 michango elfu kadhaa.

Ukweli ni kwamba watanzania wengi ni bure kabisa
 
Hizo ndiyo taratibu za kawaida kabisa, hata ndani ya GPO za Polisi zimeelezwa waziwazi.

Hata hivyo tumeendelea kushuhudia vitendo vya kihuni kabisa, vya kukamata raia wasio na hatia na baadaye tunasikia kuwa wameuawa.

Vifike mwisho vitendo hivi vya kutekana kijambazi na kihuni.

Nchi yetu inajitaanabisha kuwa ni nchi ya amani na utulivu
 
Tengenezeni Sheria inayotoa Adhabu Kali, Kwa Askari ambaye hatataka kujitamburisha wakati wa ukamataji.
 
Huo ndio usahihi....

Hizo ndizo taratibu....

Hiyo ndiyo PGO.....

#Nchi Kwanza[emoji7]
Sasa ndiyo mjuwe,kumbe wale hawakua askari na ndiyo maana hawakuzingatia PGO, wale walikua ni wahuni tu waliochukulia advantage ya upole wa watanzania ya kutii mamlaka bila shuruti!!
 
Maadili ya polisi hayafuatwi kwansababu za kiasisa, polisi ni watu wema sana ila siasa zilivyo ingilia ndio inaonekana ni wabaya kuliko hata ubaya wenyewe.
Sidhani kama mtu/polisi mwema hafuati maadili ya kazi na utu hata kama anashinikizwa kutenda jinai.Na haiwezekani kufanya jinai/utesaji na mauaji ili kufurahisha genge la wahuni na ukajiita muadilifu.Hao ni majahil wenye nia ovu tu.Hakuna cha kuwaremba au kuwakwepesha na jinai/uuaji.
 
Yeye alipokuwa ofisini alikuwa anayasimamia hayo? Au anajipayukia tuu kisa mtaafi hana wajibu wa Moja kwa Moja?
 
Kwa hali hii watekaji watanibeba nikiwa usingizini lakini kwenye basi sijui wapi wajue kabisa watafanya hivyo baada ya kuniua hadharani, utii bila shuruti kwangu haipo, yaani wanivunje kila kona ya mwili ndio wanibebe labda waje na eksikaveta
 
Kwa hiyo Kingai hakuwa Polisi??? Fikiria kabla ya kupost.
 
Wewe ukijua sheria inakusaidia nini ikiwa msimamizi wa sheria ndiye mvunja sheria? Unachokijua wewe na anachokisema huyo polisi mstaafu ni tofauti na hali halisi unayoweza kukutana nayo unapokuwa mbele ya polisi. Wale wafanyabiashara wa madini toka Mahenge Morogoro waliouawa na polisi na watanzania wakaambiwa walikuwa ni majambazi hadi ndugu zao walipoomba msaada kwa rais Kikwete na tume huru ikaundwa kuchunguza sakata lile na ikabainika hawakuwa majambazi unadhani hata wangekijua hicho unachodhani wengi hawakijui ingesaidia nini?
 
Yeye alipokuwa ofisini alikuwa anayasimamia hayo? Au anajipayukia tuu kisa mtaafi hana wajibu wa Moja kwa Moja?
We bwege askari huwa haachi majukumu

Kamishna Jamal ( Alhaj) bado anatumika jeshini kama Kachero Mshauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…