RPC Mwanza: Uhalifu ukifanyika mlinzi anakimbia

RPC Mwanza: Uhalifu ukifanyika mlinzi anakimbia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, limedhamiria kuwapa mafunzo ya utayari walinzi wa makampuni binafsi ili kuhakikisha wanatekeleza kwa weledi shughuli zao za ulinzi na kuhakikisha wanajua namna ya kutumia silaha wanazopewa kwa ajili ya shughuli zao.

Hayo yamebainishwa katika kikao maalum cha kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana na uhalifu kilichowakutanisha wamiliki wa makampuni ya ulinzi na wamiliki wa vituo vya mafuta jijini Mwanza ambapo Kamanda wa Polisi mkoani humo Wilbroad Mutafungwa, akawataka kuhakikisha wanawatengea muda walinzi wao ili waweze kupewa mafunzo maalum ya utayari yatakayowasaidia kupambana kikamilifu na wahalifu.

Wilbroad Mutafungwa.jpg

Wilbroad Mutafungwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza

"Unakuta mlinzi wa kampuni analinda sehemu, akitokea mtu anafanya uhalifu basi mlinzi ndiyo anakuwa wa kwanza kukimbia, nawaagiza wamiliki wa makampuni ya ulinzi kuhakikisha wanawatoa walinzi wao ili wapate mafunzo ya utayari kutoka jeshi la polisi ili na wao waweze kufanya shughuli zao vizuri na kuacha kujihusisha na uhalifu," amesema Kamanda Mutafungwa.

Katika hatua nyingine Kamanda Mutafungwa akawataka wamiliki wa vituo vya mafuta kuhakikisha wanafunga kamera kwenye vituo vyao ili pindi uhalifu unapojitokeza zisaidie kwenye upelelezi wa kuwabaini wahusika.

Chanzo: EATV
 
sasa nani afe kwa ajili ya mali za mtu ?😄😄😄
 
Kamanda anacheza na fursa hapa huu ni mshiko unatengenezwa tuu! Si kila polisi anao weledi wa kazi kiasi cha kuwafundisha wengine medani za ulinzi na usalama.
 
Mtu anakuja na AK47 halafu mlinzi ana Gobore au kirungu ati unamwambia apate mafunzo ya utayari! Utayari upi huo kwa mfano?
 
Siku moja majambazi yamevamia sehemu, bahati nzuri security wakapita njia hiyo tukawaambia afadhali mumetokea pale mbele kuna majambazi, basi kwa mshangao wakageuza pikipiki kurudi walipotoka, tunawauliza mbona mnakimbia, wakasema tumesahau bastola kwenye chaji tunaenda kuchukua, sasa sijui ni kiwewe au walimaanisha simu
 
Back
Top Bottom