RPC Tabora: Tunafuatilia taarifa za Wahalifu kuvamia Watu, kuwajeruhi na kupora katika Mitaa ya Chuo cha Polytechnic College

RPC Tabora: Tunafuatilia taarifa za Wahalifu kuvamia Watu, kuwajeruhi na kupora katika Mitaa ya Chuo cha Polytechnic College

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai kuwa kuna changamoto ya uhalifu maeneo ya karibu na Chuo Polytechnic College Mkoani Tabora, ambapo waathirika wakubwa ni Wanafunzi wa Chuo hicho, Jeshi la Polisi limesema linafuatilia.

Awali Mdau alieleza kuwa taarifa ya matukio ya Wanafunzi na raia kushambuliwa na kuporwa zimeripotiwa kwa Jeshi la Polisi lakini hatua hazijachukuliwa hali inayofanya waishi kwa hofu muda mwingi hasa majira ya usiku.

Hoja ya awali ipo hapa ~ Mamlaka zimeshindwa kudhibidi Vijana wanaovamia Watu, kuwajeruhi na kupora katika Mitaa ya Tabora Polytechnic College?

JESHI LA POLISI
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa, Richard Abwao amezungumza na JamiiForums kuhusu suala hilo, amesema:

Hiyo taarifa haijafika kwangu rasmi lakini mimi mwenyewe nimeiona kupitia Mitandao ya Kijamii kuhusu malalamiko hayo na tayari tumelitolea maelekezo, hatua zimeanza kuchukuliwa kulifuatilia.

Tunataka kujua suala hilo kama lipo na kwa uzito gani nak ama lipo hatua zikachukuliwa, hivyo Ofisi ya RCO (Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa) inashughulikia suala hilo kwa ukaribu.

MKUU WA CHUO CHA POLYTECHNIC COLLEGE
JamiiForums
imezungumza pia na Mkuu wa Chuo, Juma Mudini kuhusu suala hilo, amesema:

Tumefikisha taarifa hiyo kwa Jeshi la Polisi katika Ofisi ya RPC wanafahamu changamoto hiyo, tukio kubwa la hivi karibuni lilitokea mwanzoni mwa mwezi huu ambapo kuna Mwanafunzi alijeruhiwa na wahalifu hao.

Changamoto nyingine ni Wanafunzi kupenda kutembea muda ukiwa umeenda, kukitokea tukio wakati wa usiku inaweza kuwa nguvu Polisi kufika kwa wakati, lakini tumeshawaambia watembee kwa vikundi kuwa watambue muda wa kuanzia saa nne kwenda mbele sio rafiki kutembea usiku.
 
Back
Top Bottom