RT wataja Wanariadha 15 Jumuiya ya Madola, Suleiman Nyambui Kocha Mkuu

RT wataja Wanariadha 15 Jumuiya ya Madola, Suleiman Nyambui Kocha Mkuu

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Limewatangaza Wanariadha 15 wa mbio Ndefu watakaoingia Kambini (West Kilimanjaro) Kwa kujiandaa na Mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa Kufanyika Birmingham, Uingereza mwezi Agosti 2022.

Wanariadha waliotajwa ni Pamoja na Wana Olimpiki walioshiriki Mbio za Tokyo2020, Alphonce Felix Simbu, Gabriel Gerald Geay, Failuna Abdi Matanga.

Wengine ni Faraja Lazaro , Jackline Sakilu ,Fabian Nelson, Andrew Rhobi, Josephat Gisemo, Marcellina Mbua, Joseph Panga,Simon John na Ally Gulam.

Waliotajwa Wengine ni Mohamed Charles, Natalie Elisante na Winfrida Makenji.

Wakati huo huo RT , imetangaza Kocha Mkuu wa kambi hiyo ni Mwanariadha wa kimataifa wa zamani, Suleiman Nyambui akishirikiana na Msaidizi wake Kassim Salehe.

Tutarajie Makubwa.
 
Utarajie toka wapi? Wenzenu walishaanza maandalizi muda mrefu nyie ndo kwanza mnajiandaa.

Mtarudi na medali 0
 
Back
Top Bottom