Wakuu mambo vipi?
Kwanza poleni kwa msiba wa kitaifa (janga la Kariakoo).
Ishu yangu iko hivi, kuna ndugu yangu ni mfanyabiashara Dodoma. Kwa hiyo mara nyingi husafiri toka Dodoma-Tunduma na Tunduma- Dodoma kufuata bidhaa.
Anasema juzi (kama sijakosea) alikuwa akitoka Tunduma kuelekea Dodoma kwa kutumia Bus la Shabiby Line.
Anasema walipofika maeneo fulani mkoani Mbeya, basi lilipigwa mkono na mtu wa usalama barabarani ambaye baadaye walimjua ni R.T.O wa Mkoa wa Mbeya (yaani Afisa Usafiri Mkoa).
Anasema, baada ya basi kusimama, R.T.O alimwambia dereva kuwa, jana yake alifanya kosa la ku- overtake gari lingine kinyume cha sheria.
Dereva akamwambia R.T.O amuoneshe picha za gari likiwa lina overtake. R.T.O akatoa picha.
Ndugu anasema: Lakini cha ajabu, namba za basi hilo siyo za basi ambalo R.T.O alilipiga mkono.
Anasema palitokea mvutano uliyosababisha gari kusimama kwa takribani saa mbili au hadi tatu mpaka abiria wakashinikiza kwenda ofisi za mkoa kulalamika.
Huyu ndugu anaendelea kusema: Abiria tulilalamika kwamba, kama ni kweli basi letu ndilo lililofanya kosa jana yake, si ampige faini dereva kisha akaliacha basi sisi tukaendelea na safari yetu.
Hata hivyo, ndugu yangu huyo alisema amekuwa akiona matrafiki wa Mkoa wa Mbeya wakikamata sana mabasi wakati mwingine bila sababu za msingi huku kukiwa na tetesi (madai) kwamba, R.T.O anasema yeye amepelekwa mkoani humo na 'wakubwa'.
Kabla ya kuwaletea uzi huu, siku za nyuma, niliwahi kuongea na mmoja wa madereva wa mabasi yanayotoka Dar kwenda Mbeya pale Magufuli Bus Terminal, Mbezi ambaye alikiri kuwa, mabasi yamekuwa yakipigwa 'stop' nyingi mkoani Mbeya tofauti na maeneo mengine kama Pwani (Kibaha), Morogoro na Iringa.
Dereva huyo akarusha 'dongo' kwa Latra kwamba, anashangaa kuona basi moja la kampuni linapofanya kosa, wanasimamisha leseni ya kampuni nzima kusafiri, maamuzi ambayo alisema siyo sahihi.
Dereva: "Mabasi ya kampuni yangu yaliwahi kuzuiwa kwa kosa la dereva mmoja. Matokeo yake kampuni yote ikafungiwa. Dereva akafukuzwa kazi, akaajiriwa mwingine.
"Mabasi yalipofunguliwa kuanza safari, dereva mpya akapindua basi kwa sababu ya kikosa uzoefu wa barabara. Kwa nini kosa la dereva mmoja asilibebe mwenyewe badala ya kampuni?"