RTO wa Arusha namkubali

RTO wa Arusha namkubali

Wambugani

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2007
Posts
1,757
Reaction score
277
Tarehe 29 Desemba nilikuwa nasafiri kutoka Arusha kuelekea Kijiji kimoja ambacho kipo kilometa 50 kabla ya kufika Babati Mjini. Nilipofika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo Babati wapiga debe wakanipokea kwa bwembe zao
wakanionyesha tiketi zao ambazo zote zimeandikwa Sh. 6,000/= ambazo zimeshatolewa kitabuni.

Walinionyesha kiti katika basi la KANDAHAR Na. T 683 BRQ na nikawaambia kuwa kwa kuwa sifiki Babati sitaweza kulipa kiasi hicho cha Sh. 6,000/= wakakubali nilipe Sh. 5,000/=. Kwa bahati mbaya nilikuwa na noti ya Sh. 10,000/= ndipo mpiga debe akanionyesha bango la SUMATRA na kudai hakuna nauli chini ya Sh. 6,000/= na kunirudishia Sh. 4,000/= kwa madai kwamba yeye ni mwenyekiti wa SUMATRA kama sitaki kulipa kiasi hicho wanachotaka wao, nikashitaki po pote na kunitolea matusi na migambo lukuki. Kwa bahati mimi ni Nambari ya simu ya Maafisa Usalama Barabarani wa Mikoa ya Manyara na Arusha (RTO Arusha - 0658 376 076) na Manyara 0658 376 058.

Nilipompigia mara baada ya dakika takriba tano hivi, Askari wa Usalama Barabarani akaja na kuliongoza basi hilo kituoni ndipo walipolipa Notification ya Sh. 30,000/= na Sh. 1,000/= waliyotaka kunirusha nikanirudishiwa.

Rai kwa wasafiri wenzangu ni kwamba tusiwadekeze wapiga debe wanaoleta kero kwenye vituo vya mabasi na turipoti adha hiyo kunakohusika.
 
Back
Top Bottom