Rubani aliyeiba ndege ya Usovieti na kuipeleka Japan

Rubani aliyeiba ndege ya Usovieti na kuipeleka Japan

Raphael focus

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2018
Posts
779
Reaction score
4,564
Habari ya mda huu wana janvi.

Kama mada inavyo jieleza hapo juu, ungana nami AlsenetaSir katika kisa hiki cha rubani aliyeiba ndege vita ya Usovieti ya zamani .





http://cloud.tapatalk.com/s/5cfdf44d86b8c/_96162183_74fa82ea-6ef6-4a01-b79e-bc69f5593655.jpg?



Tarehe 6 mwezi septemba mwaka 1976 ,ndege ilionekana ghafla kutoka kwenye mawingu karibu na mji wa Hakodate katika kisiwa kilicho kasikazini cha Hokaido nchini Japani.



Ilikuwa ndege yenye injini mbili lakini haikuwa ndege ya kawaida ambayo watu wa Hakodate walikuwa wamezoea kuziona .


Ndege hiyo kubwa iliyo kuwa na alama za Muungano wa Usovieti haikuwa imeonekana eneo hilo kabla.

Ilitua katika uwanja wa Hakodate .Barbara ya uwanja wa ndege ilikuwa fupi hali iliyo lazimu kuchimbua aridhi , ilipomaliza kukimbia kwenye barabara na kusimama mwisho kabisa mwa uwanja wa uwanja wa ndege.

Rubani akachomoza kutoka katika chumba cha rubani na kufyatua risasi mara mbili hewani kutoka kwa bastola yake.

Dakika chache baadaye maafisa wa uwanja wa ndege wakamkaribia .Huu ndio wakati wa rubani mwenye umri wa miaka 29 Luten Viktor Belenko wa jeshi la wana hewa alitangaza kuwa alitaka kuhama.

Ndege hiyo aina ya Mikoyan-Gurevich MiG -25 ndiyo ndege yenye usiri zaidi kuwai kuundwa na muungano wa Usovieti.

Nchi za Magharibi ziligundua kitu ambacho kilionekana kama ndege ya MiG 25 miaka ya sabini. Satelaiti za ujasusi zilikuwa zikichunguza viwanja vya Usovieti zilichukua picha ya ndege zilizo kuwa zikifanyiwa majaribio ya kisiri.

Ndege hizo zilionekana kama ndege kubwa za kivita na wanajeshi wa Magharibi walikuwa na wasiwasi baada ya kuona kitu fulani chenye mbawa kubwa.


Turudi katika kisa chetu cha rubani ,raia wa Sovieti ya zamani aliye iba ndege ya Usovieti mwaka 1976 nakuitoroshea nchini japani.


Viktor Belenko alikuwa raia wa Usovieti ,ilizaliwa mara baada ya vita vya pili vya dunia eneo la milima ya Caucasus .

Alijiunga na jeshi na kufuzu mafunzo kama rubani wa ndege za kivita cheo ambacho kilikuwa na hadhi ya juu kuliko cha mwananchi wa kawaida.

Akiwa baba wa mtoto mmoja wakati huo ,huku akikabiliwa na talaka alikuwa na maswali mengi kuhusu jamii ya Usovieti.

Belenko alifahamu kuwa ndege kubwa ya kijeshi ambayo aliitumia kujifunzia ingekuwa njia muhimu ya kuitumia kukimbia .

Akiwa katika jambi ya jeshi la hewa ya Chuguyevka kalibu na mji wa mashariki wa Vladivostok. Japan ilikuwa umbali wa kilomita 644. Lakini ikiwa na injini kubwa inamaana haingeruka mbali sana hadi kutua katika kambi ya Marekani.

Tarehe 6 Belenko aliondoka na marubani wenzake kufanya mazoezi. Maramoja akatafuta njia ya kupita kwasababu ndege yake ilikuwa na mafuta ya kutosha .Alilusha ndege na dakika chache baadaye alikua safarini kuelekea Japan.

Ilikukwapa mitambo ya rada ya Usovieti na ile ya Japan ,Belenko aliluka chini kwa chini kalibu futi 100 .Lajini akipoingia anga ya Japan alipanda hadi futi 20,000 ili aweze kuonekana kwa rada za Japan .Wakati ndege za Japan zilikuwa tayali ; Belenko alitoweka na kuingia ndani ya mawingu na kutoweka kwa rada za Japan .Belenko alikuwa na nia ya kuluka hadi uwanja wa Chitose lakini ndege yake ilikuwa imeishiwa na mafuta kwa hiyo alituwa uwanja wa kalibu wa Hakodate .Ghafla Japan wakajikuta na rubani aliyehama na ndege ya kivita ambayo imekuwa ikikwepa mashirika ya Ujasusi ya nchi za Magharibi.


Uwanja wa Hokodate ukawa wenye shughuli nyingi za ujasusi jambo ambalo hata CIA haikuamini.

Hitimisho.

Belenko hakuludi USSR wala ndege yake hiyo .Aliruhusiwa kuhamia nchini Marekani baada ya kupewa uraia na Raisi Jimmy carter ampapo alipewa cheo cha mhandisi wa ndege na mshauri wa jeshi la Marekani .Kitambulisho na yale yote aliyo yaandika wakati akiwa safarini kuelekea nchini Japan yako kwenye maonyesho, kwenye makavazi ya CIA mjini Washington DC.


By AlsenetaSir.
 
Back
Top Bottom