Rubani kijana atorosha ndege

gstar

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
790
Reaction score
1,373
Kuna watu majasiri ,
Rubani kijana atorosha ndege

Rubani mmoja raia wa Tanzania anashikiliwa katika kituo cha polisi hapa Johanesburg Afrika ya kusini kwa tuhuma za kujaribu kutorosha ndege iliyokuwa imekamatwa kwa amri ya mahakama.

Rubani huyo alifika kwenye uwanja wa Oliver Tambo na kudai kuwa anataka kujaribu kuipaki pembeni ndipo ghafla alipoanza kuiendesha kwa kasi kwa lengo la kuipaisha na kuirudisha nchini Tanzania ndege hiyo ya Air Bus A220 mali ya shirika la ndege ATCL.

Ilibidi kutumia nguvu za ziada kuweza kumdhibiti rubani huyo kijana aliyekuwa na lengo la kuweka historia ya kutorosha ndege kutoka kwenye Airport ambapo ndege hiyo ilikuwa imezuiwa.

Lakini alipo hojiwa na vyombo vya habari ikiwemo CNN na BBC alikiri kufanya hivyo lakini si kwa malengo mabaya bali ni katika kupasha engine za ndege hiyo moto.

Mpaka tunaenda mitamboni kijana huyo alikuwa bado anashikiliwa na polisi wakati ndege hiyo ikiwa bado inashikiliwa bila dalili za kuachiwa leo wala kesho...

Nilikuwa naota nimeamua kushare na nyinyi hii ndoto...[emoji42]
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
hahhahahahahahaha ku ma ma ke hahahahhah
 
Kama ingekuwa kweli, basi huyo rubani angefika anapewa uwaziri kwenye wizara ileee ya bwana yuleee!

Ndoto zingine bhaana!
 
Duuuh kwaanza nimefungua kwa haraka na mbwembwe nyingi kutaka kujua jina la huyo kijana, baada ya mda nikajitukana mwenewe pumbafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…