Ruco wanafunzi wanaosomea shahada ya elimu hawajapewa pesa zao za boom miezi 5

hewa

Member
Joined
Oct 27, 2012
Posts
35
Reaction score
14
TAARIFA KWA BODI YA MIKOPO TANZANIA (HESLB) KUHUSU (RUCO)
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha RUAHA (RUCO) kilichopo mkoani Iringa, Napenda kuwajulisha kwamba viongozi wanaohusika na masuala ya mikopo hapa chuoni kwetu pamoja na uongozi mzima wa chuo wameamua kwa makusidi kabisa kutuangamiza au kuliangamiza Taifa la Tanzania bila sababu yoyote ya msingi. Hii ni kutokana na uongozi wa chuo kutulazimisha kwenda kwenye mafunzo masomoni ama (field) katika kipindi ambacho hakijazoeleka kwa wengi wetu hapa chuoni, kwa maana tulipelekwa huko field mwezi wa pili (2) na kurudi mwezi wa nne(4), sawa tulipewa pesa kwa ajili ya mafunzo hayo yaliyochukua takribani miezi kama miwili kama ilivyopangiwa budget yake kutoka bodi ya mikopo ambayo pia ilichelewa kutoka. Lakini hoja yangu kuu ni kuhusu ukata au umaskini unaotutesa tangu tulipotoka huko field mwezi wa (4) hadi leo hatujalipwa hela zetu kwa ajili ya chakula na malazi, ukizingatia kwamba siku tulizokaa hapa chuoni tayari zimezidi mara mbili ya zile siku 66 kama zinavyohesabiwa na bodi hiyo ya mikopo.mimi ninaandika ujumbe huu nikiwa na uchungu kwa sababu nateseka, nalala na njaa, masomo nayo yananihitaji chuo hawana lolote la kutusaidia serikali yetu kupitia bodi ya mikopo nanyi mumetulia sasa sijui tutakimbilia wapi, au wenda mnadhania tumesahau yale mafungu ya hela ambayo mlitupangia kila mtu kwa kiwango chake?, hata kama ni hivyo mbona bado haijatimia hata nusu yake? ngoja mimi niishie hapo maana hata nguvu za kuendelea kuandika nimeishiwa nimebakiza tu kidogo za kesho darasani
naombeni sana mtufikirie na sisi mkatuletee mafungu yetu ili, na sisi tusome na siku moja tuweze kulitumikia Taifa letu kama ninyi.Ahsante ni mimi Mzalendo Hodari.

 
Tulia wewe pesa tumetumia kwenye kumpokea Obama subiri next month mambo yatakuwa poa.Unaweza ukajibiwa hivyo ukienda kuuliza juu hii nchi acha tuu na pole sana rafiki.
 
Kumbe serikali yetu ina pesa za mchezo!yani hadi nyie nao mnapewa mikopo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…