, Inasaidia sana. Jamani mimi nilisoma shule ya Temeke. Kulikuwa na mwalimu anaitwa mwalimu Kisaka, siku ya zamu yake shule nzima ni kimya haina kelele watu ni kujisomea kwa kwenda mbele. Na shule yetu ilikua inaongoza kwenye michezo karibu yote hata kwaya na Ngoma za kienyeji. Darasani ndo usisema. Kulikua na mwalimu wa histori jina lake nimelisahau. Akikusanya madaftari usiporudishiwa ujuwe siku hiyo utafinywa au kupigwa na rula kwenye vidole hadi kesho kinaeleweka. Na matunda tunayaona kwa kweli mimi binafsi nawashukuru sana wale walimu.
Ila siku hizi mwalimu akimchapa mtoto. Mzazi anakuja pigana na mwalimu mbele ya wanafunzi wengine halafu ukute mzazi ndio ana nguvu. Hiyo picha inakuaje. Ukimkuta ana vijisenti, utakuta anampeleka mzazi polisi.
Mfano. Kuna shule nilimpeleka mwangu ya mission - huko Tanga tukakuta mzazi kwa kuwa ameambiwa mtoto wake ana wastani wa chini ya ule unaotakiwa na shule ile, aje waone jinsi gani washirikiane aweze kupanda kiwango. Yule mzazi alimtishaje yule mwalimu akamuambia nitaifunga hiyo shule na kweli alirudi Dar akaenda kushitaki Wizara ya Elimu kilichotokea hapo waliitwa wale walimu njooni mripoti wizarani haraka sana, bila kukosa siku fulani. Bila ya kujua ratiba yao ya shule ikoje. Kwenda kule wakaambwia wastani huo mnaoutaka mmeutoa wapi wakati wastani wa serikali ni 35. Bahati wale wenye shule walikua na msimamo wakawaambia sisi tunataka tutoe elimu bora kama mnataka tutoe bora elimu tuko tayari kufunga shule tugeuze kanisa.
Basi tulivyoletewa hiyo taarifa siku ya wazazi kwa kweli tulihudhunika - na watu kwa pamoja tukawasapoti wale walimu kama yeye mtoto wake ni mjinga asituletee ujinga wake hapa shuleni. Hebu aifunge hiyo shule tuone. Kwa kweli watu wakalifanyia kazi jambo lile na bado hiyo shule iko kwenye kumi bora.
Sasa ninachosema hapa, nidhamu kwa shule ni muhimi katika matokeo ya mtoto kitu ambacho watu wengi tumekisahau au hatutaki kukiangalia. Na nidhamu inatakiwa ianze kwa mzazi hadi kwa mtoto. Na utaona matokeo yake. Mbona hizi shule za seminary zinafanya vizuri. Kwa sababu wao wanazingatia nidhamu. Na wanafuatilia hadi hata wewe mzazi wakati mwingine unaona ni kero. Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu unajitahidi tu ili mtoto awe na msingi mzuri.