Rudisheni lugha ya Kiingereza shuleni kama lugha ya kufundishia

Rudisheni lugha ya Kiingereza shuleni kama lugha ya kufundishia

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Posts
2,180
Reaction score
1,291
limekuwa gumzo kwa nini mawaziri na watu wanaojiweza wanapeleka watoto wao shule za kiingereza kwa gharama kuu wakati watoto wa masikini hawajaliwi katika shule za kata. sababu ni moja tuu ni kutafuta njia ya watoto wao waongee kiingereza vizuri kama ilivyokuwa enzi za darasa la nane .sasa badala ya kupigania kiingereza kirudishwe mashuleni msingini tunalalamika. watanzania wengi wanataka kiingereza kukiongea basi tukifanyie baby comeback mashuleni.

hivi mtanzania anaweza kujiajili mwenyewe katika nchi za watu wengine bila ya kujua lugha ya kiingereza? wasanii wetu hasa wachekeshaji mbona hawaendi kokote nje ya tanzania wakati wale wa kenya, ghana na Nigeria huenda popote pale kutafuta soko na kujiingizia dinari.

Wabunge wanalalamika kila kukicha eti wahitimu wa vyuo vikuu wengi husaga rami kutafuta ajira wakati huo huo hawaoni jinsi wakenya, waghana na Nigeria walivyo sambaa sehemu nyingi duniani wakijiari na kupata kazi kwa sababu moja tuu ya kujua lugha ya jumuia ya common wealth.

tungekuwa kiingereza ni lugha ya mtanzania ya pili Bongo flava muziki wake ungependwa africa yoooote na kuvuma kama vile enzi za CAVASHA ya zaire' jamani hata CNN, FOx na bbc mtoto ashindwe kujua nini kimetokea duniani.

Hongera sana mawaziri wote na wananchi wanaopeleka watoto wao english medium maana siku moja hawatashindwa kufanya kazi za ukatibu mkuu UN, AU,kuongoza mahakama za kimataifa,kupatanisha wagombanao, na kuchezesha mechi za world cup
 
Mimi nimesema nitavaa hata magunia, lakini mtoto lazima aendelee kusoma shule ya mitalaa ya kiingereza. Hao viongozi wanajifanya wazalendo, lakini watoto wao wakiongea kiingereza wanatabasamu hadi jino la mwisho linaonekana. Nenda huko manyumbani mwao, wao na watoto wao wanaangalia DSTV na sio hizi local za michezo ya kina Mkojani. Halafu wakimaliza shule anayeajiriwa ni anayejua kiingereza fasaha.
 
... wote ni mashuhuda jinsi Kiingereza kilivyotugeuza kituko siku zilizopita. Bosi akiongea watu mnainama kwa aibu? Sio tu lugha ila hata kujenga hoja na ushawishi ni zero. Tuondokane na ujinga ule! Haiwezekani bila kuwekeza sana kwenye elimu.

Sijajua siri ya hii kitu; hivi ni kwanini watoto wadogo, mfano wawili, chosen at random, huyu yuko mtaala wa Kiswahili na huyu yuko mtaala wa Kimalkia inakuwaje yule wa Kimalkia ana confidence ya hali juu mno na uwezo wa kujenga hoja na ushawishi kuliko yule wa Kiswahili hata kama lugha watakayokuwa wanatumia ku-argue ni Kiswahili?

Hebu wataalamu wa social sciences and human behavior fanyeni tafiti zenu mlete majibu badala ya kuwaachia wanasiasa laghai wanaojifanya kujua kila kitu wananchi wanachotaka bila hata kuwauliza hao wananchi.
 
Tumedharau kiingereza na tunapoteza mno, wapo na wengine kama akina jpm waliochukia lugha hii na kuanzisha kampeni dhidi ya kiingereza ila ukweli unabaki palepale, lugha ya kiingereza ni muhimu kwa ajira za ndani au nje ya nchi ambapo kiingereza fasaha kinahitajika.
 
Elimu tuliyonayo hivi sasa ni ya kimatabaka, inatengeneza tabaka la wenye nacho na wasiokuwa nacho, inatengeneza tabaka la watawala na watwana, inatengeneza tabaka la watakaotajwa kuwa wasomi na wasiowasomi, ...rudi Mwl wa walimu Hayati Julius K. Nyerere Baba wa wote
 
Shida kubwa ni kuwa hatujawekeza vya kutosha katika elimu.. hata kama tukiamua kiingereza kiwe lugha rasmi ya kujifunzia.. je tuna waalimu mahiri wa kiingereza?
 
Shida kubwa ni kuwa hatujawekeza vya kutosha katika elimu.. hata kama tukiamua kiingereza kiwe lugha rasmi ya kujifunzia.. je tuna waalimu mahiri wa kiingereza?
Tutababaisha mwanzoni ila bàadaye walimu watapatikana wakigraduate watakaofundishwa kwa english
 
Umenikumbusha kuna mwamba humu Jeiefu alienda South Afrika (nafikiri kikazi, sina uhakika).

Ulipofika muda wa chakula akaombwa aombee chakula. Hapo ndipo tatizo lilianza😂😂😂😂😂. Kimalkia kilimpa za uso bila huruma.
 
Mkuu tango, Kiingereza kina faida gani!Waliofanikia kimaisha wengi wao hawajasoma, wengine hata kuandika hawajui.


Wewe na kiingereza chako kimekufikisha wapi?
 
Mkuu tango, Kiingereza kina faida gani!Waliofanikia kimaisha wengi wao hawajasoma, wengine hata kuandika hawajui.


Wewe na kiingereza chako kimekufikisha wapi?
Wenzio wanazungumzia jambo hili kwa mapana yake, wewe unakuja na hoja ya waliobahatisha, na hata huyo ambaye hakusoma, alisaidiwa na waliosoma vizuri
 
Ni ujinga usiomithirika kubeza lugha ya kingereza ilihali tunajua kabisa kwamba English is a Lingua Franca of many speech communities. Kubeza lugha ya malkia ni udhihirisho kuwa wewe fikra zako ni fupi kwa kiwango cha kuhuzunisha sana.
 
Hiyo Lugha ya kingereza Inaongeza vitamin zipi kwenye mwili wa binadamu??
 
Tumedharau kiingereza na tunapoteza mno, wapo na wengine kama akina jpm waliochukia lugha hii na kuanzisha kampeni dhidi ya kiingereza ila ukweli unabaki palepale, lugha ya kiingereza ni muhimu kwa ajira za ndani au nje ya nchi ambapo kiingereza fasaha kinahitajika.
Mwendazake alitaka lianzishwe somo la "Historia ya Tanzania" na lifundishwe kwa kiswahili kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita. Historia yenyewe ilikua ni kumtukuza mwendazake. Huyu jamaa alikichukia sana kiingereza. Waziri wa elimu naye alikwenda na mapigo ya muziki wa boss wake. Bado kuna watu walishangilia hii tabia.
 
Back
Top Bottom