Rudisheni lugha ya Kiingereza shuleni kama lugha ya kufundishia

Lugha ya Kiingereza ndiyo iliyotujengea Tanzania. Waliosoma kwa kiingereza ndio wamejenga barabara, hospital , shule, viwanda.vyuo, mahoteli, magorofa, Wanatibu Wagonjwa kwa Elimu ya Kiingereza waliyopata hadi wanafanya upasuaji wa moyo na vichwa, Walianzisha Mabank, Posta, Simu, Miundo mbinu ya Maji, Mpangilio wa Ofisi za Umma na Mashirika. Hawajakosea.
Banda ya kuona tumeshindwa kuandaa Waalimu wa English ndio tunaona English Shuleni haifai.
Nilisoma kijijini enzi hiyo ya Mwalimu Primary nikabahatika kwenda Secondary Masomo yote kwa English. Nilijitahidi kusoma kwa bidii Novel na kujifunza English hakuna Somo nilikuwa sielewi na kujibu maswali yake sawasawa.
 
Kiingereza mashuleni watafundishwa na nani? Maana, walimu nao hawakijui!
Kama kweli nchi inataka kuwa serious, waajiri walimu kutoka Uingereza au wapeleke walimu Uingereza wakasomee kufundisha kingereza fasaha mashuleni.
Chonde Chonde wasituletee waganda na wa Kenya! Wametuaribia kingereza!
Mfano utasikia Bathidai baada ya Beethidei (matamshi ovyo).
 
😂😂hamna namna
 
... mbona huo utafiti hauendani na uhalisia?

Fanya utafiti mdogo; randomly choose a sample of Class 4 pupils from normal English medium schools. Similarly, choose a sample of Class 4 (of similar size) from the BEST Kiswahili medium schools. Perform some tests like mathematics, writing, and reading abilities as well as confidence, persuasion, general understanding of global issues, manner, etc. on those two samples. You will probably be surprised.

Nadhani alichofanya Profesa Qorro ni kufanyia utafiti wake ngazi za juu sekondari na elimu ya juu ambapo wanafunzi tayari walishapigika na kuchanganya lugha Kiswahili (msingi) then suddenly English (sekondari). Hapo matokeo lazima yawe na walakini. Hoja ni Kiingereza kianzie level za chini hadi za juu.
 
Mkuu tango, Kiingereza kina faida gani!Waliofanikia kimaisha wengi wao hawajasoma, wengine hata kuandika hawajui.


Wewe na kiingereza chako kimekufikisha wapi?
Hao waliofanikiwa bila elimu, ni wachache kati ya maelfu na maelfu ya ambao hawakusoma, ila waliosoma angalau wana kaunafuu kidogo wa maisha
 

Nakuunga mkono hoja! Tunakosea kutupa kiingereza huku tukijua ukweli kuwa tunakihitaji katika elimu na maarifa kuliko kiswahili!!
 
Elimu yetu ni mbovu sababu ya kutumia kiingereza. Tungetumia kiswahili hadi PHD tungekuwa na elimu bora sana.
PHD ya kiswahili halafu ukafanye kazi kwenye mitubwi ya shemeji kule mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…