JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), kupinga hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, imeshindwa kuendelea baada ya mawakili wa wajibu rufaa kuomba kufanya mapitio Mahakama ya Rufani.
Leo Jumatatu Februari 20, 2023 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilipanga kuendelea kusikiliza rufaa hiyo, ambapo DPP aliwakilishwa na Mawakili wa Serikali waandamizi Felix Kwetukia, Timotheo Mmari na Hebel Kihaka.
Wajibu rufaa waliwakilishwa na mawakili Mosses Mahuna, Fauzia Mustapha, Fridolin Bwemelo na Sylvster Kahunduka.
Mbali na Sabaya wajibu rufaa wengine ni Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.
Mbele ya Jaji Salma Maghimbia anayesikiliza rufaa hiyo, Wakili Kwetukia aliieleza mahakama kuwa, Februari 3, 2023 walipokea maombi ya kufanya mapitio yaliyoandaliwa Januari 27, 2023 inayoomba Mahakama ya Rufani ifanye mapitio ya mwenendo wa rufaa hiyo na uamuzi mdogo uliotolewa Desemba 14, 2022.
"Kwa msingi huo kwa kuwa kuna maombi ya mapitio ni rai yetu rufaa hii isubiri kwa muda ikisibiri uamuzi wa maombi ya upande wa wajibu rufaa ualiyopelekwa katika mahakama ya rufani," ameeleza Kwetukia.
Jaji Maghimbi amesema kutokana na maombi hayo katika mahakama ya juu, shauri hilo la rufaa litasubiri hadi uamuzi wa mahakama ya Rufani yatakapotolewa.
Leo mbali na Sabaya mjibu rufaa mwingine aliyekuwepo mahakamani hapo ni Mnkeni, huku wajibu rufaa wawili ambao ni Aweyo na Nyegu wakiwa hawapo mahakamani hapo, ila mawakili wanaowawakilisha wakiwepo, ambao pia waliieleza mahakama kuwa hawana taarifa za Msuya na Macha.
Desemba 14, 2022 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitupilia mbali pingamizi lililokuwa limewasilishwa mahakamani hapo na mawakili wa Sabaya.
Miongoni mwa hoja ambazo mahakama imetolea uamuzi ni pamoja na kutupilia mbali hoja ya rufaa kukatwa nje ya muda pamoja na ufafanuzi kuhusu mrufani wa tatu, Watson Mwahomanhe ambaye awali upande wa wajibu rufaa uliibua hoja ya kutokuonekana mahakamani.
Uamuzi huo mdogo ulitolewa na Jaji Maghimbi ambapo Wakili Mahuna anayemwakilisha mjibu rufaa wa kwanza (Sabaya), aliwaasilisha hoja mbili za pingamizi za kutaka rufaa hiyo itupiliwe mbali.
Kuhusu hoja ya wakili Mahuna ya rufaa hiyo kuwasilishwa nje ya muda, Jaji Maghimbi amesema rufaa hiyo imewasilishwa ndani ya wakati na kuwa kwa mujibu wa sheria siku 45 za kukata zinaanza kuhesabiwa pale ambapo nakala za mwenendo wa kesi na uamuzi unakuwa umetolewa.
Amesema anakubaliana na hoja ya wakili wa serikali mwandamizi Patrick Mwita ambaye jana akijibu hoja za pingamizi hilo la awali aliileza mahakama kuwa siku 45 za kukata rufaa zinaanza kuhesabiwa baada ya kukabidhiwa nakala ya mwenendo wa kesi na hukumu.
Kuhusu hoja ya pili iliyotolewa na Mahuna akidai kuwa notisi ya nia ya kukata rufaa inatofautiana na maombi ya rufaa, Jaji amesema anakubaliana na hoja ya wakili wa serikali mwandamizi Patrick Mwita kuwa baada ya kupata mwenendo wa shauri na hukumu ndipo unaweza kuamua nani umkatie rufaa.
Chanzo: Mwananchi