KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Waombea takribani 240 wa nafasi mbalimbali, wameenguliwa kugombea katika uchaguzi huo.
Wagombea wetu waliwekewa pingamizi, na wagombea wa CCM, baadaye Chadema wakakataa rufaa, lakini kilichotokea rufaa zimegonga mwamba.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu, Mussa Onesmo akiongea anasema katika hizo pingamizi, mmoja wa wagombea aliwekewa pingamizi kuwa yeye hana shamba baada ya kujaza kuwa yeye ni mkulima.
Soma Pia:
- Wagombea wa CHADEMA waenguliwa kwenye kinyang'anyiro kisa hawana kazi ya kuwapatia kipato halali
- Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwingine kwenye fomu yake alipojaza jina la kijiji, iliongeza herufi moja mbele, Kamati haijaona hilo ni kama kosa dogo ambalo ni kama kosa la kuandishi, huyo mgombea wetu ameenguliwa na yeye.
Mwenyekiti wa chadema Simiyu anasema makosa mengi ni madogo na mengine ya kutengenezwa, lakini hakuna mgombea hata mmoja wa kwao ambaye ameitwa kwenye kamati kwa ajili ya kuhojiwa.
Mwenyekiti huyo anaeleza watakwenda kupiga kampeini hata ambako wagombea wao wameenguliwa, na watawahasisha wananchi umuhimu wa kupiga kura ya Ndiyo na Hapana.