The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Jumla ya watu 16003 wakazi wa vijiji 30 wilayani Rufiji mkoani Pwani wamenufaika na msaada wa kisheria bila malipo kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa kampeni hiyo Wilayani humo Gloria Baltazari ambaye pia ni Wakili wa Serikali anayehudumu katika Wizara ya Katiba na Sheria wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kampeni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rufiji na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Rufiji
Wakili Gloria amesema jumla ya makundi yote ya jamii yamefikiwa na kampeni hiyo kupitia mikutano ya hadhara, kutembelea shuleni pamoja na nyumba za Ibada.
Katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda wa siku 10, wananchi wamejengewa uwezo kuhusu taratibu za kumiliki ardhi kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kununua, kurithishwa na kukodi huku wakitahadharishwa juu ya njia ya kumiliki ardhi kwa kuvamia mapori kama iliyopigwa marufuku na sheria ya ardhi ya mwaka 1999.
Katika suala la ardhi, pia wananchi wamejengewa uwezo kutambua haki zao katika ardhi yao na kupewa elimu ya kisheria na njia sahihi za kutafuta haki zao kama vile usuluhishi panapotokea migogoro ya ardhi baina ya vijiji na vijiji, vijiji na mamlaka za hifadhi, na kufungua shauri katika mabaraza ya ardhi panapotokea migogoro ya vijiji na wawekezaji, mtu na serikali au migogoro baina ya mtu na mtu.
Vilevile wananchi wamepewa elimu juu ya umuhimu wa kuandaa wosia utakaotoa mwongozo wa ugawaji na usimamizi miradhi baada ya kufikwa na umauti. Katika suala la wosia, wananchi wamepata ufafanuzi kuhusu aina mbili za wosia ambazo ni wosia wa kuandika unaoshuhudiwa na mashahidi wawili ambao sio wanufaika wa mirathi.
Aina ya pili ni wosia wa mdomo unaotolewa na mtu aliyekatika hali ya kifo au wanajeshi waendapo vitani. Aina hii ya wosia unashuhudiwa na mashahidi wanne. Aina zote hizi za wosia zinaweza kubadilishwa au kufanyiwa marekebisho huku cha kuzingatia ni kwamba wosia ni siri na inapaswa kuandaliwa kwa msaada wa wanasheria na kuhifadhiwa mazingira salama kama vile mahakamani na nyumba za ibada.
Pia elimu kuhusu masuala ya ndoa na ustawi katika jamii imewafikia wananchi wa Rufiji wakihimizwa kuzingatia taratibu na sheria za ndoa za dini zao na zile za kiserikali. Katika hili wanandoa wote wameaswa kutimiza wajibu wao kwa wenzi wao na familia kiujumla ili kutokomeza matukio ya ukatili, utelekezaji wa watoto pamoja na talaka zisizo za lazima.
Aidha timu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia iliwafikia wanafunzi shuleni na kuwapa elimu namna ya kutambua viashiria vya vitendo vya ukatili, kuviripoti kwa vyombo husika na kuvitokomeza.
Pamoja na hayo yote changamoto mbalimbali za migogoro ya ardhi, ustawi wa jamii na tafsiri ya sheria zimepatiwa ufumbuzi katika mikutano ya hadhara iliyokuwa ikifanyika katika kijiji kwa kijiji huku mingine ikifikishwa kwenye mamlaka husika kwa utatuzi chini ya ufuatiliaji wa timu ya kampeni hiyo iliyosheheni wataalamu wa sheria, ardhi, ustawi wa jamii, dawati ya jinsia pamoja na maendeleo ya jamii
Baada ya kupokea taarifa hiyo mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Luteni Kanali Fredick Komba, Kaimu Mtendaji wa Wilaya Judith Mlangwa pamoja naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Rufiji Sebastian Gaganija wamepongeza jitihada kubwa zilizofanyika kuimarisha haki na sheria katika jamii na kuahidi kuendelea kufuatilia kwa karibu mashauri yaliyoibuliwa.