Rufiji na Geita zapandishwa Hadhi ,Maendeleo hayana Chama

Rufiji na Geita zapandishwa Hadhi ,Maendeleo hayana Chama

Malick M. Malick

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
658
Reaction score
312
RAIS SAMIA AZIPANDISHA HADHI RUFIJI NA GEITA.
Na Malick Maliki, Chamwino

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipandisha hadhi Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji na Halmashauri ya Mji wa Geita kuwa Manispaa.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Desemba 13, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Rufiji kwenye uwanja wa ujamaa - Ikwiriri walifurika kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la Bibi Titi Mohamed.

Amesema “Bibi Titi Mohamed huko aliko atakua anafurahia sana maendeleo ya Rufiji maana ndiye Mbunge wa kwanza aliyeasisi jimbo hili alifanya kazi kubwa sana na mimi Mbunge wa tisa naendeleza kazi aliyoianza Hayati Bibi Titi na pia Mhe. Rais amefanya kazi kubwa kwa kuleta miradi mingi katika Wilaya yetu na sasa ameipandisha hadhi kuwa Halmashauri ya Mji.”

Amefafanua kuwa hadhi ya Mji ina maana kubwa sana kwa wananchi wa Rufiji kwa kuwa itakua miongoni mwa Halmashauri zinazojufaika na miradi mikubwa ya Benki ya Dunia na maendeleo yanakwenda kwa kasi katika kila Kata masoko yatajengwa, huduma za Afya zitapatikana karibu zaidi na miradi ya elimu itaongezeka.

“Hivyo tunamshkuru Mhe. Rais kwa kuiona Rufiji na kuipa hadhi ya kuwa Mji na sasa maendeleo katika Wilaya hii katika nyanja zote yataenda kwa kasi zaidi,”amesema.

Tamasha la Bibi Titi linafanyika wilayani Rufiji kwa siku tatu kuanzia tarehe 12-14/12/2023 kwa lengo la kumuenzi shujaa Bibi Titi Mohamed kama mwanamke wa kwanza kupigania uhuru na Mbunge kwa kwanza wa Rufiji.
 
Amesema “Bibi Titi Mohamed huko aliko atakua anafurahia sana maendeleo ya Rufiji maana ndiye Mbunge wa kwanza aliyeasisi jimbo hili alifanya kazi kubwa sana na mimi Mbunge wa tisa naendeleza kazi aliyoianza Hayati Bibi Titi na pia Mhe.
INNALLILLAH WAINNAH RAAJIUN. DAH SISI WAISLAM TUMEFIKIA KUSEMA HAYA TENA. MAITI AKASIKILIZE NA KUFURAHIQ DHULUMAT ZINAZOFANYIKA DUNIANI?
 
Rufiji bado sana nilikua nweny vijiji vya mbunju,mpima,ruwe, na vingine kama nane hivi pamoja na hapo ikwiriri kwenyewe aisee ni bado sana hata sehem ya kula yenye kueleweka hakuna
Mama mkwe kampongeza mkwe wake kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye serikali za mitaa.
 
Rufiji bado sana nilikua nweny vijiji vya mbunju,mpima,ruwe, na vingine kama nane hivi pamoja na hapo ikwiriri kwenyewe aisee ni bado sana hata sehem ya kula yenye kueleweka hakuna
Mkuu,

Hukupita pande za Muhoro?

Nilikuwa huko 1995 ndiyo nikajua kuna Dar na Tanzania.
 
Rufiji bado sana nilikua nweny vijiji vya mbunju,mpima,ruwe, na vingine kama nane hivi pamoja na hapo ikwiriri kwenyewe aisee ni bado sana hata sehem ya kula yenye kueleweka hakuna
Yeah uko sahihi, kwa Geita kuwa Manispaa ni Sahihi kabisa sio Rufiji
 
Hahahhaaa mkaza mwana kazawadiwa hadhi...kwakazi zote 2.......uchaguzi na ya nyumbani kwake...
 
Back
Top Bottom