Rufiji watumia mapato ya ndani kuboresha elimu

Rufiji watumia mapato ya ndani kuboresha elimu

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Muktasari:

Ndani ya mwaka mmoja na miezi mitano Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani imefanikiwa kuweka miundombinu mbalimbali itakayosaidia kuboresha elimu wilayani humo kwa shule za msingi na sekondari.

Rufiji. Ndani ya mwaka mmoja na miezi mitano Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani imefanikiwa kuweka miundombinu mbalimbali itakayosaidia kuboresha elimu wilayani humo kwa shule za msingi na sekondari.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 13, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, John Kayombo imeitaja miundombinu hiyo kuwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za walimu na kutengeneza madawati.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitano Halmashauri imeweza kutumia fedha za mapato ya ndani kujenga, vyumba vya madarasa 30 kwa msingi na 48 kwa sekondari.

“Pia tumejenga matundu ya vyoo 132 msingi na 67 sekondari, nyumba za walimu 14 pamoja na madawati 1496 msingi na 2006 kwa sekondari,” Kayombo amesema katika taarifa hiyo.

Aidha amesema wataendelea kusimamia elimu ya msingi, sekondari pamoja na kuboresha huduma ya afya kama vipaumbele vyao vikuu.

Mwananchi
 
Wilaya zote Za mkoa wa Kilimanjaro wamehamia kuiba fedha Za Ndani na miundombinu Za shule zimeoza kabisa.

Ufanyike ukaguzi maalumu kwenye hizo wilaya kuoanisha mapato ya ndani na miundombinu ya shule Za serikali.

Hali ni mbayaaaaa sana
 
Back
Top Bottom