Kama mtu ni mfatiliaji wa muziki bas hakuna hasiyejua kuwa Clouds ni kituo kinachodidimiza wasanii wengi tu. Wanawajengea bifu wasanii kitu ambacho ni cha hajabu.
Ukwel ni kuwa kazi nyingi za show zinapitia mikononi mwa Clouds lakini si busara ata kidogo kuwanyanyasa wasanii kwa sababu hii.
Yan wanataka wasanii wajibembeleze kwao,wanachotaka au kusema ndiwe kiwe hvyo hvyo,hii haiwezekani.
Na ndiyo maana nilikuwa namuelewa sana sugu alipokuwa anapigia kelele kwa studio iliyotolewa na JK kupewa huyu jamaa Luge.
Kwa wasanii hakika Luge na Clouds hawawatendei haki,wale wasanii wa ndiyo baba ndo wanaopeta pale.
Nje ya muziki Luge na Clouds wanafanya poa,mfano kuna watu wengi sana uwa wanapewa msaada kuanzia chakula,mahala pa kulala paka wanapopata msaada kamili toka kwa wadau wengine, kuna watu wapo shule,watu wametibiwa magonjwa yao kwa kupitia Clouds haya jamaa wapo poa sana ila kwa wanamuziki hawapo sawa.