Ruge nini ulichomfanyia Q-chief?

NguoYaSikuKuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
681
Reaction score
1,020

Nimesikilza hii video ya msanii Q-chief imenisikitisha sana jinsi wasanii wazuri kama hawa wanavyopotezwa na watu fulani fulani kisa ya masilahi binafsi.

Binafsi nafkiri Q-chief ni moja ya wasanii wenye vipaji sana na mahiri kutokea hapa nchini. Najua ana mapungufu yake,ila sidhani anastahili kuwa alivyo sasa.

Nimegundua baada ya kutazama hii video.

Ruge ni mwiba sana katika tasnia ya sanaa hapa nchini,hataki mtofutiane katika maslahi yake.
 
Last edited by a moderator:
Nimemkumbuka q chillah na lisong lake "tanita". "Mboni ichafukapo jicho huwa mashakani, ni mbali we ulipo na sijui u hali gani"
 
Q chief aliwah kua juu sana hakutengeneza mazingira alijisahau,wamekuja vijana wapya ladha tofauti,ni.sidhani kama ni sahihi kumshutumu ruge,
 
aliende kukimbilia ma drugs unategemea angetokaje uko ukisha changanya drugs na kazi huezi sogea popote pale kwa tz hii na njaa kalii hii unaenda tena jichanganya kwenye matapu tapu. unajichimbia shimo mwenywe. hana maana napia akubali kila jambo na wakat wake. tupo kidigital zaidi. alikua analogy kule tusha toka. so abadilike naye.
 
mara m baya wake diamond.mara. tid anamloga sijui jafarai anamdhulumu mbona haeleweki safari hii ruge ndio source ya failure yake na downfall
 
Lord have Mercy!!
Hivi huyu Q Chilla sijui Chilla anamjua Qs Mhonda au anamsikia tu!!? Mhonda ni balaa!! Tapeli sijapata kuona!!
 
Anavuta unga na kula mirungi, gari lake ni laku supply Vitu hivyo, zamani lilikuwa huchelewi kulikuta polisi kisha linarudi uraiani tena.
 
q chief mwizi toka zamani sana kabla hajamjua ruge
japo wasanii wengi wakishaona wamepigwa chini na ruge wanapata stress na kuanza kula maunga maana jina nalo linaanza kufa tartibu
 
Kachuja mwenyewe. Ruge kamfunga mdomo? Ana sauti ila hajui ubunifu wa kuimba. Amfuate dimpoz amfundishe atoke vipi
 
Nimemsikia Chillah kwenye hii Video anasema amekuwa na msoto mkali kwa miaka mitano na sababu kubwa hasa anadai kuwa ni kupishana kauli na boss mkuu wa Mjengoni Ndg Rugemalila

Vile vile amedokeza kuwa katika kipindi hiki pia alikuwa akijihusisha na utumiaji wa madawa.ya kulevya hapa sijajua ni kwa nini alijiingiza kwenye matumizi ya madawa sijui alianza kutumia kwa sababu ya msongo wa mawazo baada ya kuchemsha kwenye gemu? au sijui ni ule usela ma..vi tu??

Lakini yote kwa yote wasanii wanatakiwa waachane na hii Kasumba ya kuweka visingizio vya kubaniwa na Ruge kila wanapoanguka kimuziki wanatakiwa wabuni njia mbadala za kusavaivu katika mziki bila kumtegemea Ruge na Clouds Fm
 
Sauti kwa mbali bado ipo..ajipange anaweza rudi akapata za kubadilishia kofia...ila huyo boss mpya ...mmmh tutasikia mengine sasa hivi....time will tell
 
Uyu ----- alipokuwa juu alikuwa na nyodo sana...Ama kweli ulimwengu ndio mama.
 
One mistake one goal.Q Chief sijui Q Chillah na wasanii wa zamani hata kama RUGE anawabani why upite on his way?Mbona jide yeye anafanya yake na anafanikiwa?Kuna wasanii wazamani Juma Nature,Suma Lee,Dudu baya hii nimifano ila wanatakiwa wabadilike na soko sasa hivi mtu hatakiwi hateseki kama zamani studio 2 sijui ratiba ya kutoa wimbo miezi kibao.Siku hizi quality studio kila kona bei za kurecord ndogo.Ni mpangilio ndio maana dogo 1 song hilo hilo anahit mpk ananunua GARI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…