Kanyafu Nkanwa
JF-Expert Member
- Jul 8, 2010
- 850
- 103
Kwa hakika kitendo cha Serikali kuamua ku-centralise mambo ya kuomba ruhusa kwenda nje ya nchi kinatuvuruga sana sana. Suala la kwamba kila mfanyakazi wa serikali ni lazima apewe ruhusa na IKULU kama akitaka kwenda nje ya nchi ni kitendo kisichokubalika kabisa na usumbufu uliopitiliza. Sasa imekuwa kawaida kwa wafanyakazi kutoka mikoani kuomba ruhusa kwa immediate bosses wao ili wapeleke hizo barua Wizarani. Mimi ninachoshindwa kuelewa ni:
1. Hivi hii serikali haikupata nafasi ya kutambua kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wao kusafiri kwenda nje ya nchi ni sehemu ya kazi zao? Mtu kama huyu itabidi awe anashinda Dar es Salaam kupeleka barua za ruhusa?!
2. Serikali haioni kuwa matumizi ya fedha ya umma yataongezeka sana kwa kitendo cha watu kulipa perdiems kwenda Dar es Salaam kufuatilia hizo barua?
3. Hivi serikali haikuona kuwa itakuwa ni upotezaji mkubwa wa muda kwa watu kupanda safari za kufuatilia barua zao badala ya kufanya kazi za kawaida za serikali?
Mh. Balozi Idd hii strategy uliokuja nayo ili kudhibiti matumizi mabaya ya safari za nje inaweza kuwa kinyume na hayo matarajio. Ikibidi kama ni lazima basi ziwekwe centres mikoani ili watu waweze kuzitumia hizo badala ya usumbufu uliopo sasa hivi kwa kweli.