Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Watu wanne mkoani Rukwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kumuua kwa kumkata kwa panga ndugu yao Mashaka Sichone, mkazi wa kijiji cha Kalepula, wilaya ya Kalambo ambaye alikuwa Katibu wa CCM Tawi la Kalepula. Baada ya kufanya ukatili huo walitenganisha kichwa na kiwiliwili kisha kuondoka na kichwa chake.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) tukio hilo lilitokea tarehe 27 Januari 2025 ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Shadrack Masija amesema kuwa watuhumiwa hao waliamini Mashaka Sichone alihusika kumuua baba yao kwa kumroga.
Soma Pia: Rukwa: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Watu hao walipanga njama ya kumuua ikiwa ni sehemu ya kulipiza kisasi lakini kwa jitihada zilizofanywa na jeshi la polisi tumewakamata, na kupitia mahojiano walithibitisha na kutupeleka walipotupa kile kichwa", amesema ACP Masija