Rukwa: Lijualikali amewapiga marufuku Walimu kulima mashamba ya shule kwa manufaa yao binafsi

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Mkuu wa Wilaya Nkasi, Peter Lijualikali amefanya maamuzi magumu kwa kuzuia Waalimu kulima mashamba ya shule kwa Matumizi Yao binafsi na kutaka mashamba hayo yatumike kulima mashamba ya shule Ili waweze kupata Mahindi yatakayowezesha Wanafunzi kupata chakula shuleni.

Maamuzi hayo ameyafanya kufuatia ziara yake anayoifanya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekekezwa na serikali baada ya kufika shule ya sekondari Chala na kukuta shule hiyo imelima hekari mbili tu za shule wakati shule hiyo inazo hekari 180 ambazo Walimu wamegawana huku maeneo mengine wakiyakodisha kwa Wananchi.

Alisema kuwa wilaya kwa sasa ina mpango madhubuti wa kuhakikisha Watoto wanapata chakula shuleni na mkakati uliopo ni kuona maeneo ya ardhi yanayomilikiwa na shule kuhakikisha kwamba yanatumika kuzalisha chakula cha kutosha na kuondoa usumbufu kwa Wazazi wa Wanafunzi ya kuchangia chakula shuleni wakati shule zenyewe zinazo uwezo wa kuzalisha chakula.

Mkuu huyo wa wilaya alifadhaika baada ya taarifa iliyotolewa na mkuu wa shule hiyo ya sekondari Solo Willium ambaye alidai kuwa katika hekari 180 zinazomilikiwa na shule hiyo ni nyingi wamegawana Walimu wenyewe wanazitumia kwa kilimo na nyingine wameikodisha kwa Wananchi huku shule ikilima hekari mbili pekee kitu ambacho hawawezi kumudu kuwalisha chakula shuleni hapo kwa mwaka mzima.

Hivyo aliitumia nafasi hiyo kutoa katazo kwa shule zote za msingi na sekondari zilizopo wilayani Nkasi Walimu kutogawana mashamba hayo ya shule Wala kuyakodisha kwa jamii Hadi wapate kibali kutoka kwake,huku akiagiza shule zote ambazo Walimu wamelima mashamba ya shule watoe orodha Yao iende ofisini kwake mara Moja kwa ajili ya maamuzi mengine zaidi.

Akitoa ufafanuzi juu ya mkakati wa chakula shuleni alidai kuwa shule nyingi wilayani Nkasi zinazo maeneo makubwa kwa ajili ya kilimo na kuwa rasilimali hiyo kama itatumika vizuri inaweza kufanikisha kupatikana kwa chakula shuleni mwaka mzima bila ya Wazazi kuchangia chochote
Pamoja na hayo pia aliwataka Watendaji wa serikali kuwa waadilifu kwenye usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayote
 
Huyu kijana, Zamani alikua mzee sana..🤣
Ebu mwenye ile picha ya zamani mapema kabisa Mbowe akimnadi, aiweke hapa tafadhali..🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…