KERO Rukwa: Maafisa biashara wanafunga biashara kijiji Korongwe wilayani Nkasi bila kusikiliza changamoto za wafanyabiashara hao

KERO Rukwa: Maafisa biashara wanafunga biashara kijiji Korongwe wilayani Nkasi bila kusikiliza changamoto za wafanyabiashara hao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nipo mkoa wa Rukwa wilaya ya Nkasi kijiji cha Korongwe. Leo asubuhi kumezuka taharuki kijijini hapa KORONGWE iliyotokana na kuwepo kwa watu wanaojitambulisha kuwa ni maafisa biashara kutoka wilayani Nkasi. Wamekuwa wakizunguka ovyo mitaani kufunga biashara yaani kuweka makufuri kwa wafanyabiashara wasio na leseni/walio na leseni zilizopita wakati, licha ya Serikali na Rais kutoa katazo mara kadhaa kufungia biashara ili kuwepo mazungumzo ya changomoto kwa wamiliki wa biashara.

Kero kubwa zaidi ni hawa maafisa kudai faini(Tsh 50,000/Tsh 80,000 hadi tsh 100,000 kutegemeana na aina ya biashara) ya kuchelewa kukata leseni ya biashara, bila kutoa control namba za kulipia faini na bila kutoa risiti. Maafisa hawa wamekuwa na tabia hizi kwani hata mwaka jana walikuwa wakifungia biashara kwa makufuri na kudai faini pasipo kutoa risiti za electroniki wala control namba.

OMBI KWA SERIKALI (MAMLAKA HUSIKA)

1. Maafisa hawa wakatazwe mara moja kudai rushwa na kufungia biashara za wananchi,kwani kwa kufanya hivyo wanajenga chuki kati ya serikali yao na wananchi. (Waruhusu mazungumzo yafanyike na watoe muda/deadline ili wafanyabiashara wakate lessen). Au watoe risiti za electroniki kwa faini wanazokusanya, ili zifike moja kwa moja serikalini,kuliko kushibisha matumbo yao licha ya kupata mishahara na posho za serikali.

2. Kijiji cha KORONGWE, kipo mwambao mwa ziwa Tanganyika uchumi wa huku huendeshwa na uvuvi wa samaki na dagaa (Ziwa limefungwa mwezi wa tatu sasa tangu 15/05/2024 hakuna shughuli za uvuvi) uchumi na mapato kwa wananchi wa huku vimeshuka.

Serikali ya wilaya ya Nkasi wangetoa Muda ili kuwapa raia/wananchi muda wa kutafuta kodi za serikali ikiwemo kulipia leseni.
 
Rais Samia juzi kasema tulipe hivyo vikodi ili kuijenga nchi. Cha msingi tafuteni leseni au renew ili kuondokana na usumbufu.
 
Back
Top Bottom