Rukwa: Raia wanauza vitambulisho vya kupiga kura kwa siri

Rukwa: Raia wanauza vitambulisho vya kupiga kura kwa siri

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa, Jacob Mtalitinya amewaonya wananchi wanaouza kadi zao za mpigakura kwa siri. Amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Mtalitinya ambaye pia ni Mkurugenzi Manispaa ya Sumbawanga alisema hayo alipozungumza na HabariLEO jana katika mahojiano maalumu kuhusu kadi hizo za kupiga kura.

Alisema kuwa zipo taarifa kuwa kuna baadhi ya wananchi wameanza kuuza kadi hizo kisirisiri. Alisema wananchi hao ni wenye sifa ya kupiga kura Oktoba 28 kwamba wamejiandikisha katika daftari la mpigakura.

"Nawaomba wananchi wasiuze viparata (kadi za mpigakura) vyao, ni kinyume cha sheria kwa kuwa ni mali ya aliyejiandikisha kwenye daftari la mpigakura ...vitunzeni kama mnavyotunza vitambulisho vyenu vingine, msirubuniwe hakuna utaratibu wa kuuza, kununua au kuazimana viparata ... Msiwaachie rafiki zenu wala wenza wenu,"alihadharisha.

Alisema amelazimika kutoa hadhari hiyo, kutokana na taarifa baadhi ya watu wanapita nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa wakivichukua viparata hivyo, baada ya kuwahadaa wamiliki.

"Lipo linasemwa watu wanauziana kisirisiri, tunakusanya ushahidi ...hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika,"alisisitiza.

Alisema hadi sasa vyama vyote sita, vinafanya kampeni zao za uchaguzi kwa amani na utulivu, vikinadi ilani zao za uchaguzi kwa wapigakura wao.

Vyama vya siasa vinavyofanya kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Sumbawanga Mjini ni CCM, Chadema, CUF, ACT - Wazalendo na NCCR-Mageuzi.

"Vyama vitano tayari vimezindua rasmi kampeni zao za uchaguzi isipokuwa chama cha UDP," alifafanua.

HabariLeo
 
Watanzania wote tuna jambo letu oktoba 28. Jambo letu ni kumpa kura zote Lissu.
 
Huu mchezo wa kijinga CCM huwa wanaufanya kila wakati halafu hata hauwasaidii, mwisho wa siku lazima waibe kura, na safari hii hawaibi, wameshaambiwa watu hawataki tena mambo ya kihanithi.
 
wanauza bei gani na mimi nikachukue changu mapema ?
 
Na Mtalitinya ni mwana CCM; hawa wasimamizi watawezaje kusimamia kura huku wakiwa wa chama tawala?
 
Huo mchezo sio huko tu na huku Dsm upo unaendelea hususani katika jimbo la ukonga na sio kwa kificho uko wazi kabsa soon nitapandisha video za viongozi wanaohusika na michezo hiyo.
 
Huo mchezo sio huko tu na huku Dsm upo unaendelea hususani katika jimbo la ukonga na sio kwa kificho uko wazi kabsa soon nitapandisha video za viongozi wanaohusika na michezo hiyo.
Nangojea
 
Ni aibu kubwa kwa wanauza na wanaonunua, hawafai kuwa viongozi, uongozi ni haki,usitumia ujinga wa watu wako kujinufaisha Bali waelimishe, kama utaanza kununua haki za watu saa hizi pia utaziuza pindi ukiwa kiongozi, hili tulikemee wote bila kujali vyama
 
Back
Top Bottom