Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mwezi Julai, kituo cha uwekezaji nchini(TIC) kilitoa takwimu mbalimbali kuhusu hali ya uwekezaji nchini huku Rukwa ikishangaza kwa kuongoza kuwa na uwekezaji mkubwa zaidi. China imeendelea kuwa nchi ya kigeni inayowekeza zaidi nchini huku sekta ya kilimo ikitia fora kwa ukubwa wa mtaji uliowekezwa.
UWEKEZAJI KULINGANA NA MIKOA
Takwimu za TIC zimeuweka mkoa wa Rukwa kinara kwa kufanyika uwekezaji wenye thamani ya dola milioni 225 ukifuatiwa na Dar es Salaam($79.3M) huku Mwanza akifunga tatu bora($43.5M). Pesa zote kwa mkoa wa Rukwa ziliwekwa kwenye mradi mmoja uliotoa ajira 510 huku Dar miradi 15 ilifanyika na kutengeneza ajira 1233 na Mwanza miradi sita ilitekelezwa na kuzaa ajira 4242.
WAZAWA NA WAGENI KATIKA UWEKEZAJI
Upande wa wamiliki wa miradi hii ya uwekezaji, takwimu zinaonesha uwekezaji kutoka kwa wazawa unaendelea kuporomoka ambapo July 2022 ulikuwa 61.9% na kushuka mpaka 30% July 2023. Miradi ya pamoja kati ya wazawa na wageni imeimarika sana katika kipindi cha mwaka mmoja.
UWEKEZAJI KISEKTA
Uwekezaji kulingana na sekta, sekta ya uzalishaji(Viwanda) imeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya miradi ya uwekezaji kwa kuwa na miradi 21 kati ya miradi yote 40 sawa na 52.5% ikifuatiwa na sekta ya majengo ya kibiashara(8) huku kilimo, utalii na usafirishaji zikifungana kwa kila moja kuwa na miradi 3
SEKTA ZILIZOAJIRI WATU WENGI
Sekta ya viwanda imeakisi miradi yake ya uwekezaji kwa kuweza kuajiri watu 5793 kati ya watu 7689 katika miradi ya mwezi Julai sawa na 75.3% ya waajiriwa wote.
SEKTA ILIYOWEKEZWA MTAJI MKUBWA
Pamoja na sekta ya kilimo kuwa miradi mitatu pekee lakini inaongoza kwa kupokea mtaji mkubwa zaidi wa dola za kimarekani 228.8M sawa na 53.5% ya mtaji wote uliowekezwa ikifuatiwa kwa mbali na sekta za viwanda, majengo na usafirishaji.
MATAIFA YA KIGENI YALIYOWEKEZA ZAIDI NCHINI
China imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza bila kuyumba huku mataifa mengine yakiingia na kutoka tatu bora.