Rule number 6; "Stop Contempt" 'Acha Dharau'

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
RULE NO6; "Stop Contempt" ACHA DHARAU.

Anaandika, Robert Heriel

Nakuomba, jitahidi usome yote. Ni ujumbe utakaokufaa mpaka wajukuu zako;

Oooh! Watu wachoyo, ooh! Wanataka wafanikiwe wenyewe, oooh! Hawatupi mbinu na Siri za kutoboa. Ooh! Hatuna Pesa za kulipia vitabu au kwenda shuleni, wengine mpaka humu JF wanataka kujiua.
Taikon sitokutoza hata shilingi moja yako, labda utake ziada(nikuchapishie kitabu basi utalipia gharama za uchapishaji)

Hata hivyo isihesabike nilijitafutia utukufu, au heshima, au faida yoyote Ile kupitia mambo haya. Bali iwe sehemu ya kusudi langu la kuwapo Duniani, naam kuwapa nuru waliogizani, kuwatoa shimoni wahitajio msaada, kuwapa maarifa na hekima, na Ujuzi, na ufahamu wale watafutao mambo hayo.

Naye kila ajuaye haya asijitafutie faida Kama hakutozwa Kwa faida, hata hivyo sitoingilia Uhuru na maamuzi ya mtu Kwa maana hiyo nayo sio kazi yangu.

Niite Taikon wa Fasihi, Kutoka Nyota ya Tibeli, yenye mbawa mbili irukayo toka ulimwengu mmoja mpaka mwingine.

"Stop Contempt" naam Kwa kimatumbi ndio "Acha Dharau" hiyo ni moja ya Kanuni ya sita Kati ya zile kanuni 24 za maisha.

Ni kweli binadamu anambavu 24 ambazo hujishikiza katika UTI wa mgongo wake.
Ni kweli kila upande unambavu 12 ambapo huunda Hesabu ya mbavu 24.
Ni kweli mbavu na uti wa mgongo ndio humpa kiumbe mhimili.
Ni kweli Mbavu na Uti wa mgongo ndio huunganisha mwili, kuanzia kichwa kiwiliwili na miguu.
Hakuna anayebisha kuwa mbavu ndio huzuia viungo nyeti vilivyopo eneo la kiwiliwili Kama Moyo na Ini.
Mbavu 24 ndio huleta kanuni 24 za maisha zitakazomsaidia mwanadamu yeyote.

Mbavu ya sita Leo ndio Taikon itanishugulisha kuzungumzia. "Heshima"
Kinyume cha heshima ni "Dharau"
"Stop Contempt" Acha Dharau nikimaanisha kuwa na heshima.

Katika Dharau kuna mambo Yafuatayo;
i. Kujidharau
ii. Kudharauliwa.
iii. Kudharau.

Kudharau kunahusu mambo makuu mawili
1. Sheria
2. Imani/ uaminifu.

1. Sheria.
Msingi Mkuu wa heshima umejengwa katika sheria.
Bila sheria hakuna heshima. Kukiuka sheria ni kumaanisha "kudharau"
Kudharau ni kupuuzia iwe Kwa makusudi au isiwe Kwa makusudi sheria Fulani.

Sheria zipo Kwa ajili ya kulinda mahusiano ya watu. Hata hivyo watawala ndio huweka sheria na sio Watawaliwa. Kwa nini?

Watawala ndio huweka sheria Kwa sababu wao ndio wanauwezo wa kuzisimamia na kuhakikisha zinatekelezeka Kwa hiyari au Kwa lazima.

Mfano no1
Mwanadamu hawezi mtungia Mungu sheria hii ni Kwa sababu Hana uwezo wa kumshinikiza Mungu afuate sheria hizo.

Mfano no2
Mwanamke hawezi mtungia mwanaume sheria Kwa sababu hana nguvu ya kumlazimisha mwanaume azifuate sheria hizo.

Ila mwanaume anauwezo WA kumtungia sheria mwanamke na akafuata Kwa sababu uwezo wa kuhakikisha na kusimamia sheria hizo anao iwe Kwa hiyari au Kwa lazima/kipigo.

Mfano no3.
Wananchi hawezi itungie serikali sheria Ila serikali ndio inatungia wananchi sheria.
Mfano no4
Muafrika Kwa Zama hizi hanauwezo wa kumtungia Mzungu sheria Kwa sababu Hana uwezo wa kumshinikiza kuzitekeleza..

Kikawaida sheria hazitungwi kwaajili ya watawala Bali kwaajili ya watawaliwa.

Kimantiki, Tabaka la juu haliwezi kudharau tabaka la chini bali tabaka la chini ndilo litaitwa linadharau tabaka la juu Kwa kutofuata sheria zilizowekwa.

Tabia ya tabaka la juu itakayojitokeza inayofanana na Dharau huitwa KIBURI.
Tabaka la chini haliwezi kuwa na Kiburi isipokuwa Dharau.

Mfano, Kesi ya Daudi Vs Goliath
i. Kitendo alichoonyesha Daudi ni Dharau dhidi ya Goliath.
ii. Kitendo alichoonyesha Goliath ni Kiburi dhidi ya Daudi
iii. Kitendo alichoonyesha Goliath ni Dharau dhidi ya Mungu wa Waisrael.

Zingatia;
i. Kutoshika sheria za Wakubwa wako huitwa Dharau.

ii. Kutofuata sheria ya Jambo Fulani ni kudharau Jambo hilo hivyo huwezi kulipata.
Mfano, Ili upate elimu itakupasa usome hiyo ni SHERIA.
Usiposoma tafsiri yake umedharau hiyo Elimu. Hivyo huwezi kuipata sio ajabu wengi walifeli Shule.
Mfano no2;
Ili upate Pesa itakupasa Ufanye kazi na kuzalisha kitu Bora kinachotatua matatizo ya watu wengine.
Kutokufanya kazi tafsiri yake umeidharau pesa, hivyo hutopata Pesa.
Zingatia kupata pesa sio ufanye kazi ilimradi Hasha, bali kazi uifanyayo lazima iwe na products za uhakika zinazotatua matatizo ya watu wengine.
Katika Kazi kuna kanuni kuu tatu;
i. Kazi Bora
ii. Product Bora
iii. Bei na Muda Bora
Kanuni hizo tatu zinaunda kitu inaitwa uaminifu na nidhamu.

Acha kudharau sheria kwa kila ulifanyalo.

2. IMANI/ UAMINIFU.
Unaweza kufuata sheria za Jambo Fulani watu Kwa nje wakawa wanaona unaliheshimu Jambo Hilo lakini Kwa ndani ukawa hauliheshimu.
Sheria za ndani ndio huitwa Imani/uaminifu.
Kutofuata sheria za ndani/Imani huitwa Dharau ya ndani.

Hii IPO hivi;
Mfano No1.
Mtu anafanya kazi Fulani, anafuata sheria zote la kazi hiyo lakini haiamini kama itamfanikisha.
Unakuta mtu anafanya kilimo, analima nafikiri mfano anafuata sheria zote za kilimo lakini nafsini mwake haamini kama kilimo hicho ndicho kitakachomtoa. Hiyo inaitwa Dharau. Kudharau unachokifanya.
Na unajua nini matokeo yake?
Matokeo yake hutopata mazao, yaani hautavuna mavuno mengi, na Kama utavuna basi itatokea tatizo jingine la kushuka thamani ya zao Hilo sokoni, hayo ni matokeo ya Dharau za ndani.

Elewa haya,
i. Sheria za ndani/Imani inahusu roho na miungu Kama sio Mungu Mkuu.
ii. Sheria za nje inahusu mwili/matendo na akili zetu.

Lazima hayo yote yafanye kazi Kwa pamoja Kwa uwiano sawia. Kimoja kisimzidi mwingine.

Kutokuwa na Imani ni kumdharau Mungu au miungu. Zingatia Hakuna binadamu asiye na Imani. Huyo binadamu hayupo na hatakuja kuwepo. Hata atheist wanaimani fulani, kama wanajiamini wao kama wao tafsiri yake ni kuwa wao wanajiona ni miungu watu, wanajiabudu na kujisujudia.

Bado hujanielewa? Sidhani Kama sieleweki maana natumia lugha nyepesi ya kawaida Kabisa.

Ukienda Jeshini,
Kitu cha Kwanza utakachofundishwa na Nidhamu, kisha utapewa Mafunzo ya kuvuta na mapigano, utafundishwa saikolojia ya adui, mazingira n k.
Baada ya kupewa hayo yote cha mwisho utapewa Imani/ kujiamini, ujasiri, uhodari na uhakika wa kupigana na adui yeyote hata bila ya kuwa na silaha.
Hilo ndio Jambo kubwa kuliko yote.
Mwanajeshi bila ya Imani hawezi itwa mwanajeshi.

Dharau ambazo unapaswa kuziacha;

a). Epuka kujidharau.
Jikubali, jiheshimu. Fanya yaliyobora Kwa wakati wako.
Tumia mwili, akili, hisia na roho Kwa heshima.
Ndio maana kuna sheria, usiukosee wala usikubali Mtu akukosee mwili, akili, roho na hisia zako.
Kujiheshimu ndio tafsiri inayoelezea kujipenda,
i. Kula vyakula vizuri na sahihi, hii itakusaidia kuishi maisha mazuri yasiyo na magonjwa.
ii usikubali viingizi vya taarifa kwenye mwili wako kuingiza vitu vibaya na takataka. Heshimu macho yako, masikio yako, ulimi wako, pua yako, na ngozi yako.
Jiheshimu. Acha Dharau.

iii. Uheshimu mwili wako, uvike mavazi mazuri, usiuache uchiuchi kama Mnyama au Mbwa.
Binti yangu usikubali akili yako au mtu akataka ukae uchi mahali pasipo sahihi. Wewe sio mnyama. Wewe ni mwanadamu mwenye akili, unayejiheshimu na kujipenda.
Sio uvae linguo linaonyesha lichupi au maungo yako ya siri. Jiheshimu.

iv. Heshimu viungo vya uzazi vitakavyopitisha uzao wako.
Usizini hovyohovyo kama mwendawazimu, jiheshimu. Wewe sio mbwa kila dume likupande. Kila mwanaume aje amwage mauchafu yake kwenye Uke wako.
Hilo ni lango la pili la mwanadamu kuja Duniani lazima uliheshimu. Lazima uliheshimu. Baada ya lile lango la Kwanza la kiroho.
Kijana usitombe tombe hovyo wanawake, sio kila shimo uingize Mbolo yako. Jiheshimu, iheshimu Mbolo yako.
Kuwa Mtakatifu, maana ya utakatifu ni kuji heshimu.

v. Heshimu maumbile yako.
Uwe mfupi au mrefu, mweusi au mweupe, mwanamke au mwanaume, unakibamia au unamhogo, Una papuchi kubwa au ndogo, kuiheshimu, jikubali, jipende. Wewe ndiyo huyo sasa. Hakuna mwingine anayefanana na wewe. Usitake kuwa mtu mwingine. Usitamani Mali ya jirani yako. Tafsiri yake, jiheshimu, jipende, jikubali.
Sema moyoni; najipenda.
Kutoheshimu maumbile yako ni kujidharau, na kamwe usikubali kujidharau.

vi. Heshimu unachokifanya/kazi yako.
Kila kazi ni njema, iwe kushona viatu, kupiga Debe, Bodaboda, Kufua Samaki, Udaktari, ualimu, kazi ni KAZI.
Kuheshimu kazi yako ni kuheshimu utu wako, kuheshimu kazi yako ni kuheshimu kazi za watu wengine. Kuheshimu kazi yako ni kutafuta kuheshimiwa.

Usiwe na akili fupi, hakuna kazi Bora kuliko kazi nyingine. Kazi zote ni Sawa Kwa maan lengo la kazi ni kupata riziki na kuhudumia watu.
Mtu yeyote mwenye kudharau kazi Fulani ujue huyo hajiheshimu, Hana akili na Uelewa wake kuhusu maisha upo chini. Amezidiwa akili na Wanyama.

vii. Heshimu Mali zako
Kazi ndio itakufanya upate Mali na kuzihudumia. Hata kama ni kidogo, hata kama zinaonekana ni mbaya. Wewe ndiye wakuzifanya zionekane nzuri na zenye thamani.
Penda wazazi wako,
Penda watoto wako,
Penda Mkeo/mumeo
Penda makazi yako, yafanye yawe Safi yenye heshima, usikubali Mtu akaja na matakataka yake akayaingiza katika himaya yako, usikubali.
Penda Mali zako, mavazi, nyumba, magari, simu yako, n.k


b) Epuka kudharau watu.
Kujiheshimu ni kujali mipaka yako na mipaka ya watu wengine.
Kamwe usimdharau mtu.
Maisha yanatabia ya kukufundisha Kwa namna ya kushangaza. Unayemdharau Leo amini ipo siku utafundishwa kuheshimu watu wa Aina hiyo Kwa namna ya kipekee kama sio wewe basi utaona Kwa mtoto au mjukuu wako.

c) Epuka kumdharau MUNGU.
Kujiheshimu mwenyewe ni kumheshimu Mungu.
Kuheshimu watu ni kumheshimu Mungu pia. Hiyo ndio huitwa sheria/Torati
Kumuamini Mungu/Imani hiyo ndio huitwa Injili.

Kitendo cha kutokuwa na uhakika wa kesho tafsiri yake ni kuwa unamdharau aliyekuumba.
Lazima ujifunze na umfundishe mtoto wako kumuamini na kumtegemea Mungu pekee yake. Hiyo ndio Heshima na Kicho Kwa MUNGU.

Kitendo cha kutokuamini ati hautofanikiwa tayari kinaeleza kuwa wewe unadharau mbaya Kwa Mungu wako.
Hivi Mungu aliyeumba Mbingu na Ardhi, hii dunia unayoiona unaichukuliaje, kwamba mafanikio yako yatazidi ukubwa wa hii dunia ilivyoumbwa, kuwa serious Ndugu.

Hata hivyo elewa kuwa mafanikio ya mwanadamu hatapimwi Kwa Yale ayapatayo isipokuwa yanapimwa Kwa Yale ayafanyayo Kwa watu na Dunia Kwa ujumla.

Taikon nipumzike sasa,
Andiko hilo ni bure,
Kwa wanaohitaji ziada vitabu vilivyopo,

1. Funguo 7 milango 12
2. Mbavu 24 Rule 24
Kwa wapenzi wa Riwaya za kijasusi;
1. MLIO WA RISASI HARUSINI
2. Wakala wa Siri
3. Kaburi la mwanamuziki.
Vitabu vyote BEI ni Tsh 15,000/=
Unaweka Oda ndio vichapishwe.
Namba ya muamala
0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel

Ni yule Kuhani kutoka Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ujumbe mkubwa natumaini Makonda atapita apa kusoma na kuendelea kujifunza.
 
Umesomeka
Umeeleweka
Nimekuelewa
 
Andiko lenye maudhui yaliotukuka.
Vitabu vinapatikana soft copy?
 
Aliye Huru ni nani;-?

Mtoto anayeenda kwa viboko au mlokole mtenda mema baada ya kutishiwa moto!?

Au
Msomi ambaye elimu mpaka chuo kihakiki?


Chagua kufa ukiona waja hawalipi wema,
Kufa wokovu, kilichokufa hakifi tena,

Ukikombatia mwanga, jua utaificha Nuru,



Usikombatie uhuru wa kuambiwa, wakati unaishi na hakuchagua kuzaliwa.

Uhuru sio kufanya maamuzi.
Na
Ukishaujua uhuru tayari ushaupoteza.
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Imekaa vizuri,, mstar wa mwisho pasua kichwa
 
Imekaa vizuri,, mstar wa mwisho pasua kichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…