Rungu la TFF lamsubiria kiungo wa Kagera Sugar

ZionGate

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
6,362
Reaction score
2,991
Juzi wakati Simba Sports club ikitafuta miwa ya Kagera Sugar kisawasawa, kiungo wa Kegera Sugar Gift Mauya alimchezea rafu za Makusudi zaidi ya moja kwa wakati mmoja mchezaji wa Simba Ibrahimu Ajibu baada ya kushindwa kuuchukua mpira miguuni mwa Ajibu.
Mchezo huo usio wa kiungwana ulipelekea tafrani kubwa kwani haikuishia hapo kwani nohodha Tshabalala alikoswakoswa ngumi ya uso kutoka kwa wachezaji wa kagera baada ya wachezaji wa Simba kutokubaliana na mchezo huo. Refa alikuwa akichezesha mchezo huo aliishia kutoa kadi ya njano kwa Gift kitu ambacho kilionyesha kushindwa kumudu mchezo huo kwani kiuongo huyo wa Kagera alistahili kadi nyekundu kwa kukusudia kucheza rafu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja baada ya kushindwa kumnyang'anya ajibu mpira.
 
Asante kwa taarifa
 
Yule dogo anaitwa Zawadi Mauya. Nasikia ameshaomba msamaha. Na kwa kuwa Refa alishampa adhabu ya kadi ya njano, na pia alitelekezwa na Baba yake mzazi na kisha kupewa zawadi kwa mama yake, hivyo naishauri TFF imsamehe bure. Chenga za Ajibu na Kipigo cha 3:0 ndio kilimfanya apaniki.
 
Nilishangaa refa kwann hakutoa kadi nyekundu alikusudia kumuumiza Ajibu anastahili adhabu
 
Mikiaaa mechi ya Kagera ni mechi ndogo sana wala sio ya kuandikia mauzi kibao
 
Nguvu mlizotumia kujiandaa kushinda mechi dhidi ya Kagera Sugar, mngetumia walau nusu yake tu dhidi ya UD Songo, muda huu mngekuwa mnatafuta nafasi ya kuingia hatua ya makundi klabu bingwa Afrika!

Sasa angalia, mmerudi mlikotoka! Mbumbumbu fc!
 
Nguvu mlizotumia kujiandaa kushinda mechi dhidi ya Kagera Sugar, mngetumia walau nusu yake tu dhidi ya UD Songo, muda huu mngekuwa mnatafuta nafasi ya kuingia hatua ya makundi klabu bingwa Afrika!
Sasa angalia, mmerudi mlikotoka! Mbumbumbu fc!
Bila shaka nyie mmesonga mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…