Rupia: Hazina ya Mjerumani

Ishu za zebaki nazo ni upigwaji mwingine
Jamaa yangu aliingizwa mkenge na mmasai aliyejifanya mshamba kabisa... Akijifanya katokea ngorongoro na kaikinga hiyo zebaki kwa miaka mitano...ikamtoka laki 2 na gharama za gesti
Unajua unapokuwa desperate na utajiri utalishwa matango pori mengi sana
 
Aliingia ktk hayo mashimo alipofika kulikuta hilo sanduku lenye fedha akamtokea mdada mrembo akamsalimia ...anko akashindwa kujibu basi yule mdada alikaa kwa dkk kadhaa akatoweka anko alivotoka kule ktk shimo tu hakuchukua muda akafa
Mmh wapi huko
 
Mshana katika hili naamini hujalifanyia uchunguzi wa kutosha au leo umemuachia mtu akuandikie wewe upo Kanisani.

Kwanza Vita ya Pili Wajerumani walikuwa hawapo washaondoka vitu vilizikwa kabla ya Vita ya kwanza

Pili utaratibu wa kuficha vitu kwa kuzika pamoja na watu hai umekuwepo Ulaya Siku zote na ndicho walichofanya na zege nyingi tunazovunja sehemu hizo unakuta kabisa mafuvu ya watu waliokufa kwa kulazimishwa ( kawekewa zege miguu tuu au kichwa tu)
 
Nikubali marekebisho kwenye vita pengine ni kweli....hayo mengine umekosea sizungumzii watu waliozikwa na vitu. Wala makaburi nazungumzia mali zilizofichwa ikiwemo pesa za rupia ...hebu rudia kusoma tena kwa makini nilichoandika
 
Eneo moja mbeya tukuyu mwakareli inasemekana jamaa walificha mali kwenye ceiling board kanisani na lile kanisa wakati wanaenda kufunga msalaba juu mfungaji mzungu aliporomoka hadi kufa. Mpaka leo msalaba haukukamilika kamesimama kamoja tu kawima.
Walirudi kwa mbwembwe ya kufumua cealing board wakarabati waliishia kufumua na kubeba mali zao wakatembea. Habari yako ina element nyingi za ukweli.
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…