Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Tunaoishi sasa tunaamini tuna akili kubwa na maarifa mengi kuliko walioishi kale, jambo ambalo siyo kweli.
Naamini watu wa kale walikuwa na akili kuliko tunaoishi leo. Kwenye maarifa, kwa sababu maarifa huwa ni mwendelezo kutoka aliyetangulia alipoishia, hivyo yalipofika leo ni mbele zaidi kuliko hapo kale.
Watu wa zamani walikuwa na akili zaidi kuliko wa sasa kwa sababu waliiona kesho kabla haijafika.
Kule kwenye biblia, mtu mwenye hekima kubwa kuliko wanadamu wote, mfalme Sulemani, anasema RUSHWA HUPOFUSHA.
Mkiwa vipofu mnafanana katika kutoona. Yawezekana kabla ya kupofuka, mmoja alikuwa anaona wastani, mwingine anaona kidogo,mwingine alikuwa anaona sana, mwingine alikuwa anaona kwa kusaidiwa na miwani. Kwa hiyo kabla ya kupofuka mnatofautiana sana katika uwezo wa kuona. Lakini mkipofuka, wote mnafanana, wote mnakosa uwezo wa kuona.
Kwenye hoja ya bandari, ukimsikiliza Musukuma, Mbarawa, Nape, Kibajaji, Japipo, mwansheria wa wizara, kama hujaambiwa backgrounds zao, huwezi kujua kama miongoni mwao kuna wa darasa la saba, profesa, wa degree moja au wa darasa la nne. Wote wamefanana. Utofauti wao wa kuona umesawazishwa.
Nadhani kitu kimojawapo kinachojali sana usawa, rushwa ni miongoni maana inawafanya mfanane bila ya kujali utofauti wa hali zenu za zamani.