Wanajanvi ni imani yangu mko slalama, nimeingia katika jukwaa hili kutahadhalisha rushwa iliyotamalaki katika taasisi za fedha yaani benki na nyinginezo. Mara ya kwanza nilishuhudia hili katika taasisi moja ya Microfinance ambayo iko mkoani Arusha. Mke wangu alishatimiza masharti yote ya kukopa pamoja na kupeleka viambatanisho, cha ajabu yule afisa mikopo akawa anachelewesha mambo akitaka kitu kidogo ndo mkopo utoke. Mke wangu aligangamara mwishowe mkopo ulitoka bila kutoa rushwa ingawa ilimchukua muda mrefu.
Mimi binafsi miezi mitano iliyopita niliomba mkopo katika benki moja ambayo sitaki kuitaja jina kwa sasa, nimeshamaliza taratibu zote zinazotakiwa lakini cha ajabu siambiwi kama nimequalify kupata mkopo au la. Nilipomwambia jamaa yangu juu ya jambo hili akanicheka sana akasema kwani wewe umewaambia za kwao ni ngapi? Nilistuka sana nikasema pamoja na riba zilivyo kubwa kumbe unatakiwa kuwahonga maafisa mikopo wa benki? Akasema huo ndo utaratibu wa sasa ulivyo katika taasisi za kifedha.
Wanajanvi napenda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha kwamba rushwa imetamalaki ndani ya benki zetu, wamiliki wa benki hizi wanatakiwa kumulika rushwa hii la sivyo maendeleo ya nchi yanacheleweshwa na hawa wala rushwa ambao siku ukishindwa kulipa ndo hao wa kwanza kuja kupiga mali zako mnada huku wakikucheka bila kujali kama uliwapa kitu kidogo.