Rushwa, kukosesha Halmashauri, Manispaa na Majiji kipato

Rushwa, kukosesha Halmashauri, Manispaa na Majiji kipato

Shujaa Nduna

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2022
Posts
599
Reaction score
487
Jamani kuna halmashauri,majiji pesa za serikali zinapigwa si kitoto,wakubwa nao wapigaji huku chini itakuwaje jamani?

Nimeita halmashauri moja kanda ya kusini nikasajili kikundi cha wakulima ajabu wenzangu walienda mara2 kufatilia cheti na risiti lakini walikuwa wanaambiwa tutawaletea cheti huko nyumbani.

Nilishikwa na butwaa inakuwaje malipo ya serikali mtumishi atapeleka cheti home na control namba hakutowa na hakika cheti alipeleka na akapewa cash.

Nilihoji sana mwisho nikapotezea mana mi mgeni wenyeji hawashtuki.Wakati mwingine nikaenda kulipia leseni ya biashara nikawb dokument wakaniambia gharama lakini nikaona hata hawafanyi kazi,nikawaulizaa vipi wakasema mtandao.

Nikaona isiwe kesi nikaacha details tukapeana cmu namba ili mtandao ukiwa sawa nirudi,lakini hawakupiga mwisho jioni natoka mazoezini naambiwa wameleta risiti ya malipo na dah.Yani mtumishi wa serikali anapelekaje document nyumbani au kazini wakati mwenye dokumeti ndiyo inabidi afate?

Halafu wanakuwaga na wakala wao wa kulipia wanakueleza kwa fulani sijuwi wamapataga visenti?Naishia hapa mwenye macho na aone.

Nashauri idara za upelelezi zifanye upelezi kwenye maofisi yote nchi nzima na wakati mwingine wajifanye wahitaji wa huduma mtajuwa kadhia hizi siyo wanakuwa wapelelezi kwenye kesi za kusingiziana uwizi wa kuku.Nchi inapoteza mapato.
 
Back
Top Bottom