Rushwa kwenye chaguzi CCM zinatia kinyaa

Rushwa kwenye chaguzi CCM zinatia kinyaa

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,396
Reaction score
4,080
CCM imejikita kwa kutumia makada wake kina Kibajaji, Msukuma, Kigwangala na Kihongosi kumsema na kumtukana balozi Bashiru badala ya kuzijibu hoja zake kwa umakini.

Wakati huo huo CCM ipo kwenye uchaguzi wa viongozi wake nchi nzima uchaguzi uliotawaliwa na utoaji wa rushwa wa kutisha kwa wanaotaka kuchaguliwa kwa wapiga kura.

Kwa mujibu wa katiba ya CCM inamtaka kila mwanachama aahidi kuwa

"Rushwa ni adui wa haki sitatoa wala kupokea rushwa"

Lakini ahadi hiyo haitekelezwi kwa vitendo na CCM ipo kimya.

Nilitarajia kwa kuwa CCM ndio chama tawala kingeonyesha mfano kwa vitendo kukitumia chombo cha Serikali TAKUKURU kuwakabidhi wanachama wake waliojihusisha na utoaji na upokeaji wa rushwa kwa chombo hicho ili wafikishwe mahakamani lakini CCM inaishia kufuta chaguzi.

Kwa mtazamo wangu suala la rushwa tena ktk chaguzi ni hatari sana kuliko malumbano ya CCM na Bashiru.

millardayo_1669089578978863.jpg
 
Mbona wewe hujatoa hizo hoja za Bashiru unaruka ruka tu.
 
 
Kimsingi hao wanaompamba wa kuupiga mwingi wanasahau kuwa wanaua chama Chao. Kwasa hata zile slogans za chama hazitajwi tena. Anashanihizwa mama tuuu
 
Kwenye kumbi za CCM huwezi kusikia mtu anatamka neno rushwa sababu wote wanaingia kwa rushwa.
 
Back
Top Bottom