Rich Dad
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 748
- 135
HII nchi inakokwenda sijui ni wapi? PCCB wamelala usingizi mzito. Hawana msaada wowote kusaidia kukomesha katabia ka baadhi ya wafanyakazi wa hizi kampuni za simu zenye kuuza laini za uwakala kinyume cha taratibu. Unakuta mtu kakamilisha taratibu zote za usajili, lakini kinachotokea hawa jamaa wana ku-delay makusudi ili uwakatie kitu kidogo. Kwa sasa hawa jamaa wanataka TZS 100,000 hadi TZS 300,000 kwa laini moja.
Ukijifanya wewe ni mtu wa kufuata taratibu basi jua itakuchukua zaidi ya miezi sita kupata laini. Kila siku utapigwa kalenda kwamba kuna hiki na hiki kinakosekana. Sasa hivi TiGo wanatumia mgogo wa TCRA kwamba ndio wanaobania watu wasipate laini, lakini ukigawa chenji .....fasta ndani ya siku moja au mbili unakuwa umepata line.
Haya nayasema si kwamba nimehadithiwa, ni kwamba yamenikuta mimi mwenyewe.
Wadau naombeni tu mnipe taratibu za nani nimuone pale TiGO na Voda ili niwasilishe barua yangu ya malalamiko pamoja na vithibitisho kwa jinsi rushwa inavyokwamisha juhudi za watu kujikwamua na umaskini.