Mtu wa kati
Member
- Jul 16, 2022
- 5
- 4
Tasnia ya Habari ni miongoni mwa Tasnia zenye Hadhi kubwa katika Taifa letu. Waandishi wa habari na Vyombo vya habari ukiwa ndio mhimili mkubwa kabisa wa sekta hii muhimu ya kupashana habari.
kadri miaka inavyozidi kwenda na teknolojia kukua ndio sekta hii inavyozidi kudidimia badala ya kukua,kuna athari kubwa sana ya uwepo wa mitandao ya kijamii na maendeleo ya hii kada.
Kuna wakati tulifika mbali sana kwa kutaka kuwa vyombo vya habari kuwa ni mhimili mmoja wapo wa dola.
Lakini niwe muwazi tu waandishi wa habari wakiwa ndio mhimili mkubwa wa hii kada ya habari wameamua kujikaanga kwa mafuta yao wenyewe.
Kupenda rushwa kwa kiwango cha juu ni miongoni mwa sifa kuu za hawa watu walio wengi japokuwa wapo wachache waliosafi.
Habari nyingi zinazoripotiwa zina harufu ya rushwa,hakuna Natural Justice za kubalance story kwa kuhoji pande zote mbili na mengineyo mengi.
Urafiki na kujuana nalo ni changamoto sana,wazazi maskini wengi wa kitanzania waliwekeza nguvu kubwa sana kusomesha watoto wao ili wawe kama kina Shabani Kisu, Salim Kikeke na kina Charles Hilary wapya lakina cha kushangaza ni washehereshaji kama kina Zembwela, Masanja na Mpoki ndio wameshikilia hizi nafasi, ndio usishangae sasa hadi machawa nao sasa ni sehemu ya waandishi wa habari.
Hivi vitu vimepelekea baadhi ya watu kuidharau hii kada na kupelekea sekta ya habari kuyumba.
Tukio la jana ni sehemu tu matokeo ya muda mrefu sana ya namna mnavyojiendesha na kujichukulia na watu wanavyowachukulia nyinyi. Kanuni rahisi ya maisha ni vile unavyojichukulia na watu ndio wanavyokuchukulia.
Kalamu na Midomo yenu kwa sasa inatumika vibaya kwa wengi wenu.
Hamchezi nyimbo za wasanii wachanga mpaka mpewe rushwa,mnachagua habari ipi isomwe na ipi isisomwe kwa manufaa yenu binafsi.
Mmekuwa ni watu wa kusifu tu vile mnavyovipenda pasipo kukosoa.
Msichokijua ni kwamba hadhira yenu imepungua kwa kiasi kikubwa sana,watu wengi wamebaki kupenda kuona au kusikiliza vipindi vichache tu kutoka kwenu.
Sheria mpya ya habari ingemulika vitendo hivi na pia kusaidia kuondoa rushwa katika vyombo vya habari kwani inawanyima wananchi haki yao ya msingi ya kuhabarishwa na kujieleza na kupata habari.
Wamiliki wa Vyombo vya habari inabidi waajiri wanahabari kwa taaluma na uweredi wao na wala sio umaarufu na uchawa wao.
Kilichotokea kiwe chachu cha kuheshimisha tasnia yenu na sio kunungunika kwenu hakitawasaidia kitu chochote zaidi ya kutaka watu kuelewa nini kimewakuta na kuanza kuwacheka.
Inukeni,jifuteni na kuanza kusimama imara.
Kiuhalisia hoja ya kuwa kuna waandishi wa habari wapya na wazamani mliitengeneza wenyewe kwa kuendekeza rushwa,urafiki na kujuana.

Upvote
1