Pre GE2025 Rushwa ya ngono inavyowatesa wanawake wanaotaka Uongozi

Pre GE2025 Rushwa ya ngono inavyowatesa wanawake wanaotaka Uongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Oct 8, 2024
Posts
8
Reaction score
5
Rushwa ya ngono ni matumizi mbaya ya madaraka ili kujinufaisha kingono visivyohalali au pasipokuwa na makubaliano ya pande zote mbili.

Kwa mujibu sheria ya kuzuia Rushwa na Uhujumi Uchumi Zanzibar nambari 5 ya mwaka 2023 kifungu cha 52 kimekataza rushwa ya ngono kwa kumtaka mtu mwengine afanye ngono na, kosa hilo adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 7 au kisichozidi miaka 10.

Licha ya sheria hiyo kuwepo lakini, utekelezaji wake bado unasua sua kwani hongo ya ngono haichukuliwi kuwa ni unyanyasaji na inaonekana kama ni makubaliano baina ya watu wazima wawili na kupuuza kwa matukio ya aina hiyo hususan kwenye siasa.

Aina hii ya unyanyasaji imeenea hasa wakati wa uteuzi wa ndani ya vyama na kipindi cha uchaguzi ambapo viongozi wanaume hulipa upendeleo wa rushwa ya Ngono kwenye suala la nafasi za uongozi kwa wanawake.

Serikali ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa kama mkataba wa CEDAW ulioanzishwa mwaka 1979 na lengo lake ni kupinga aina zote za udhalilishaji dhidi ya wanawake.

Hidaya (ambaye sio jina), 55 mtoto wa mwisho katika familia ya watoto 7,mama wa watoto watatu anayeishi na mume wake hapa Kisiwani Unguja anasimulia safari yake ya siasa na rushwa ya ngono ilivyoua ndoto ya kuwa diwani.

Hidaya* ambaye alianza siasa miaka ya 90 ila kadhia ya rushwa ya ngono kwake ilinukia mwaka 2010 ambapo aligombania rasmi nafasi ya ujumbe kamati ya siasa ngazi ya shehia, lakini hakubahatika. Hakukata tamaa ilipofika 2015 alijaribu tena kuingia katika ulingo wa siasa na kugombea nafasi ya mkutano mkuu Mkoa na pia udiwani kupitia kwenye jimbo lake. "Mwaka huo ulikuwa ni wa mikosi kwangu kwanza nikaikosa nafasi ya Mkutano Mkuu Mkoa na pia kutakiwa kimapenzi na mtu wa karibu” Anasimulia Hidaya*

"Siku moja majira 12 jioni tunarudi kufanya kampeni tukiwa sehemu haina nyumba alinionesha hali ya kutaka kunibaka, na kuniambia haya ni malipo yangu kwako kama unataka nikusaidie upate uongozi "Anasimulia Hidaya huku akionekana kuwa na aibu ya kusema tukio hilo ambapo mtu aliyekuwa kama familia alimtaka kingono.

"Yalitolewa maneno ya uongo dhidi yangu licha ya kupambana nikashindwa hatika hatua ya awali kwenye kura za maoni" Hii inaonesha dhahiri kuwa ni baada ya kukataa rushwa ya ngono na kupelekwe kwenye kamati ya maadili kwa utovu wa nidhamu ili kuweza kutafuta mwanamke waliomuwezesha kifedha agombee ili amshinde na kufanikiwa kwa mbinu yao hiyo nae kukosa.

Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 inaonesha Zanzibar ina watu 1,889,773 kati ya hao wanaumme ni 915 ,492 na wanawake ni 974 ,281 hii ina manisha kwamba wanawake ni asilimia 51.6 ya wakaazi wote Zanzibar.Licha ya wingi huo bado kumekuwa na upungufu wa wanawake kushiriki katika uongozi kutokana na vikwazo tofauti vikiwemo rushwa ya ngono.

Katibu wa Uenezi Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar Khamis Mbeto amesema CCM kinahamasisha wanawake kugombea nafasi za uongozi na kuwataka wagombee wasikubali kutoa rushwa ya ngono kwa manufaa ya kuchaguliwa au kupata nafasi."Wanawake wanatakiwa wajiamini wawe na uthubutu wasiyumbishwe na mtu kwani sio lazima utowe rushwa ya ngono ili upate uongozi na Chama Cha Mapinduzi kinakemea na kulaani masuala ya ngono na udhalilishaji wa wanawake"Amesema Mbeto akiwa Ofisini kwake Kisuwandui.

Simulizi ya Hidya* ni mfano wa visa vingi vya rushwa ya ngono kwenye vyama vya siasa ila sio wanawake wengi wenye nguvu ya kutoa taarifa au kusema kwa kuogopa kuabika na hata ndoa zao kuvunjika na jamii kuwatenga.

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Siti Abass Ali amesema rushwa ya ngono ni kitu cha siri na hutokea katika maeneo tofauti wanawake lazima watoe taarifa juu ya matukio hayo ili wanaofanya wachukuliwe hatua na kujulikana "Suala la ngono ni kitu nyeti na ni aibu kusema moja kwa moja mbele za watu na wengi wanaofanyiwa huficha na kuwaficha hii inabeba utu wa mtu ila nawaomba wanawake waseme na kukemea mambo haya kwa nguvu zote "Amesema Siti kwa kusisitiza kuwepo kwa madawati ya jinsia ambayo yatatoa nafasi kusikiliza wagombea wanawake wanaopitia kadhia ya rushwa ya ngono wakati wa uchaguzi.

ChamChcha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania upande wa Zanzibar –TAMWA-Z Zanzibar, katika Ripoti yao June 2024 inayohusu uchambuzi wa ukatili dhidi ya wanawake katika vyama vya siasa Zanzibar imeeleza kuwa washiriki wa utafiti walirekodi visa vya ukatili wa kijinsia ni asilimia 21.88% na hakukuwa taarifa za kuripoti matukio hayo.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar – ZEC kupitia kupitia Mkurugenzi wake Thabit Idarus Faina amesema ya Tume ya Uchaguzi ina sera jumuishi ya jinsia ambao inashajihisha wanawake kuingia katika uongozi wakiwa salama bila ya kuwepo kwa rushwa ngono ya au fedha."Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ina sera jumuishii ya jinsia ambapo wanashajihisha wanawake kuingia katika uongozi na nikiri kwamba hatujawa kupokea kesi za udhalilishaji kwani kesi hizo zinapelekwa polisi" Amesema Faina akihitimisha mazungumzo yake.
Hadia Ali Makame ni mmoja mwanamke aliyewahi kugombea Udiwani katika kijiji cha Mkokotoni Mawimbi Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskizini Unguja amesema wanawake kuweka wazi suala la rushwa ya ngono ni aibu kutokana na mila na desturi za kizanzibar

“Tukikaa pamoja tunasema chini kwa chini ila mtu kutoka hadharani kusema ni ngumu maana itakuwa ndo kushajivua nguo” Amekiri kwa kuongezea kuwa "Rushwa ya ngono ipo na inaumiza mwanawake na hutumiwa na wanaume kama ni daraja na kumvukisha mwanamke upande wa pili" Amemaliza Hadia.
 
Kuna ule msemo wa hovyo sana wa ukitaka cha uvunguni, sharti uiname! Mimi kwa kweli siwezi kumruhusu bibi yenu aingie kwenye siasa!
 
Back
Top Bottom