Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007(PCCB Act, 2007); Rushwa ya ngono ni pale ambapo mtu aliye katika mamlaka na katika kutekeleza mamlaka yake akitaka au akiweka upendeleo wa ngono kama kigezo cha kutoa ajira, cheo, haki, au huduma ya upendeleo.
Na akifanya hivyo atakuwa amefanya kosa, na ataadhibiwa kwa faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo cha miaka isiyozidi mitatu au vyote kwa pamoja.
Iwapo utakutana na mkasa wa namna hiyo toa taarifa katika ofisi ya TAKUKURU iliyo karibu nawe au piga simu namba 133.