Russia Great Wip

Russia Great Wip

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
JOSEPH STALIN NA VLADIMIR PUTIN, NI WAJEURI, WABABE NA MIAMBA INAYOFANANA URUSI, NI STALIN ALIYEINGIA IKULU YA KREMLIN KWA NGUVU, NA NI PUTIN ALIYEINGIA KREMLIN KWA KULAZIMISHWA LAKINI ANAYETAMANI KUWA RAISI WA MAISHA.

Comred Mbwana Allyamtu
Wednesday-24/10/2018.
Marangu, Kilimanjaro- Tanzania

Shirikisho la Russia (Russia federation) ni taifa linalotokana na Ile iliyokuwa muungano wa Kisoviet uliovunjika rasmi mwaka 1991, Urusi au Russia Kama inavyo fahamika ni miongoni mwa mataifa yenye Uchumi unaoinuka kwa kasi duniani huku ikishika nafasi ya pili duniani kwa kuwa taifa lenye nguvu ya kijeshi nyuma ya Marekani. Pamoja na hivyo Russia bado ni taifa lenye uwezo mkubwa zaidi kwenye technology ya kijeshi ulimwengu kuliko taifa lingine lolote lile.

Russia Federation kuna dini mbili kubwa ambazo ni Wakristo wa madhehebu ya “Orthodox” ambao wengi wanapatikana Kaskazini Magharibi mwa Russia na katikati mwa Russia (Siberia), na dini nyingine kubwa ni Uislamu ambayo ipo kwa wingi maeneo ya Caucus na maeneo ya katikati Magharibi mwa Russia (Kazan). Hizi ndizo dini kuu mbili zinazo kubalika zaidi Russia na Serikali imekuwa haina pingamizi lolote la dini hizi mbili.

Pia Rais Vladimir Putin ni rais pekee wa Ulaya Mashariki ambaye amepiga marufuku vitendo vyote vya ushoga katika nchi yake, Ushoga nchini Russia ni kosa la jinai ambalo ukipatikana nalo unafungwa jela kwa miaka mingi. Katika siasa septemba 2011, Urusi ilifanya Marekebisho ya Katiba yake katika kipengele cha muda wa rais kukaa madarakani. Marekebisho ya kutoka miaka minne hadi sita na Putin akatangaza kuwania madaraka ya urais kwa mara ya tatu katika uchaguzi uliofanyika Machi 2012. Toka hapo Putin amekuwa mbabe akitangaza Urusi yenye mabadiliko ya kweli katika kila sekta badala ya kuwa na serikali isiyo na mamlaka.

Hii ndio Urusi ( Russia ) taifa linaloongoza kwa ukubwa wa eneo duniani. Lina ukubwa wa kilomita za mraba 17,075,200 milioni sawa na maili 6,592,800. Ni kwamba nchini Urusi majira ya saa yanayotumika katika taifa hilo ambalo ni taifa moja linalotumia majira kumi na moja (11) tofauti ya saa ( time zones ). Yani ukiwa ndani ya Urusi maeneo Kumi na moja hupishana majira,Tukiachana na kuifahamu Russia au Urusi katika siasa, tamaduni na geographia yake sasa tuludi mpaka katika viunga vya jijini la St Petersburg mwanzoni mwa miaka ya 1910.

Mwanzoni mwa karne ya 19 Katika Chama cha Kikomunisti, kulikuwa na vijana wanne wenye maono na itikadi za kikomunisti ambao ni Leon Trotsky, Joseph Stalin, Grigory Zinoviev na Lev Kamenev vijana hawa walikuwa watu walio aminiwa mno na mwanamapinduzi wa kikomnist Vladimir Erich Lenin katika harakati za ukombozi na mapinduzi ndani ya chama cha kikomnist cha Bolshevik.

Hatimae mwaka 1917, Urusi au Dola ya Umoja wa Nchi za Kisovieti ikiwa chini ya uongozi wa itikadi ya ukomunisti, huku Vladimir Lenin akiwa ndio kiongozi wa kwanza wa taifa hilo kubwa, vijana hao wanne waliingizwa kwenye chombo kikuu cha uamuzi katika chama na Serikali (Politburo) kutokana na kuaminiwa na mchango wao katika mapinduzi ya mwaka 1917 kama wajumbe saba waanzilishi wa chama cha Bolishevik pamoja na dola la umoja wa Soviet (Soviet Union).

Katika vijana hao mmoja wao aliyeitwa Joseph Stalin alionekana kuwa mbabe,mwenye mikakati mingi kuliko wenzake watatu. Stalin alipenda kuwashinda wenzake na aliweka mikakati mikubwa ya kuwa mtawala wa taifa hilo kubwa la kirusi au Soviet Union.

Kwa warusi jina la Joseph Stalin si rahisi kusahaulika,Stalin ndie aliyerithi mikoba ya Vladimir Elich Lenin kwa kuwa rais wa pili wa Soviet Union, Ni mtu ambaye miaka mingi iliyopita alionekana kuwa mwenye roho ya kinyama lakini hivi karibuni katajwa kuwa shujaa wa taifa hilo. Joseph Stalin ni kiongozi aliyeifanya Urusi kuwa dola kubwa lenye kuongoza dunia ya kijamaa na tishio duniani kwa kile kilichotazamwa kama zama za ulimwengu wa nukria (almagadoni).

Ni Stalin aliye anzisha mpango wa urutibishaji wa madini ya uranium kwa utengeneza wa makombora ya nukria, pamoja na miradi mikubwa ya uchumi ndani ya Urusi, huyu Stalin alikuwa na misemo mingi Katika uhai wake lakini aliyopenda kuisema ni hii " kifo ni suruhisho la matatizo . kama hakuna binadamu hakuna matatizo." Lakini pia alipenda kusema "simwamini mtu yeyote ,hata mimi mwenyewe".

Jina Stalin linamanisha " Mtu wa chuma" kwa kirusi, kutokana na jina lake kweli alikuwa ni kiongozi shupavu na katili kweli kwani Inakadiriwa kuwa katika uongozi wake watu zaidi ya milioni 20 waliuawa kutokana na kupinga utawala wake pamoja na wale walio onekana kama maadui wa Urusi na wengine wanaofikia milioni 14.5 walikufa njaa hii ilitokana na Mageuzi ya uchumi ya 1925-35. Huku idadi ya watu milioni moja inakisiwa kuwa ilipotea kwa kunyongwa kwa sababu za kisiasa, Pia idadi nyingine Laki tisa wakape lekwa uhamishoni au kufungwa kwenye kambi za mateso . wengi waliopelekwa huko hawakurudi hai.

Joseph Stalin ni tofauti na wanamapinduzi wengine kwani yeye aliusaka uongozi kwa nguvu zote toka mwanzo na alitumia akili nyingi kufanikisha malengo yake, toka mwanzo akiwa mfuasi wa Lenin alianza kuwekeza mikakati ya kufanikisha malengo yake. Hata hivyo Stalin na Trotsky walikuwa watu wa Karibu sana na Lenin mwasisi wa Urusi. Tofauti ya Stalin na Trotsky ni kwamba Trotsky alimuunga mkono Lenin waziwazi tofauti na Stalin, Trotsky alionekana kijana mwenye akili nyingi, maana baadhi ya nadharia zake za kiuongozi, zilitumiwa pia na Lenin. Watu wengi Urusi wakati huo, waliamini mwisho wa Trotsky ungekuwa kuongoza Dola ya Kisovieti baada ya Lenin.

Wakati Trotsky akionesha mapenzi kwa Lenin na kuwa mfuasi wake mtiifu, Stalin alikuwa akimpinga Lenin pembeni kwa kuunda ngome za chini chini lakini mbele za macho alijionesha kuwa hakuna anayemkubali Lenin kama yeye. Stalin hakumpenda Trotsky na alimuona ni mtu hatari kwa maslahi yake ya kisiasa na malengo yake ya kumrithi Lenin baadae, kwa hiyo akawashawishi wenzake ambao ni Gregory Zinoviev na Lev Kamenev wakaunda utatu wa kisiasa na kidola ambao waliuita Triumvirate wakiwa na malengo ya kujitanua kisiasa ndani ya umoja wa kisoviet yote.

Stalin na wenzake walijiita Triumvirate wakijilinganisha na utatu wa Julius Caesar, Pompey na Crassus wa dola ya Roma ya kipindi kile cha kale, ambao umoja wao huo waliounganisha nguvu ili kuitawala Roma, miaka 60 Kabla ya Kristo ambao hufahamika kama The First Triumvirate na ule wa Anthony, Lepidus na Octavian unaofahamika kama The Second Triumvirate, miaka 43 Kabla ya Kristo. Na huu wa Joseph Stalin, Gregory Zinoviev na Lev Kamenev unajulikana kama third triumvirate wa miaka ya 1920 lengo lao ilikuwa ni kutawala Urusi lakin kabla awajatawala lazima wahakikishe Trotsky wanammaliza kisiasa Maana Trotsky ndie aliyeonekana tishio katika ustawi wao hasa Stalin.

Stalin taratibu akaanza kushinda njama zake huku Trotsky akajikuta kwenye mapambano na Triumvirate Ile ya Stalin na wenzake wawili. Stalin hakuwa na ushawishi mkubwa, hivyo aliwatumia Zinoviev na Kamenev kumshughulikia Trotsky kwenye chama na serikalini akijua iwapo Trotsky atashughurikiwa na kumalizwa basi njia ya Stalin itakuwa nyeupe kuelekea Ikulu ya Moscow ya Kremlin. Kufatia hatua hiyo ya kuitumia propaganda vyema hatimae Trotsky akaitwa msaliti jina likakua na umma ukaaminishwa hivyo.

Baada ya Trotsky kupungua nguvu ndani ya chama chake na kwa umma wa kisoviet, Stalin aliwageuka Zinoviev na Kamenev akawachachafya kuwa nao ni wasaliti hatimae na wao wakachafuka na Ile triumvirate ikapasuka vipande. Wakati wote huo Lenin alikuwa mgonjwa hivyo vuta nikuvute ya kugombania nani atakua mrithi wa Lenin ilikuwa kubwa, hata hivyo Stalin alifanikiwa maana Aprili 3, 1922, Stalin alikamata mamlaka ya chama cha Kikomunisti cha Bolsheviks baada ya Lenin kuachia madaraka ya chama ingawa ulitokea mzozo mkubwa maana sehemu kubwa ya wanachama walikuwa bado wanamwamini Trotsky wakimtazama kama Lenin mwingine. Kufatia mgogoro huo chama kikaingia kwenye mpasuko wa makundi.

Baada ya Stalin kukamata nafasi hiyo Stalin bado aliendelea kumhofia Trotsky, hivyo alizidi kumchafua alihakikisha anatambulika rasmi serikalini kama msaliti kwa jina la msaliti Trotsky, yaani Msaliti Trotsky. Vyombo vya habari vikamwita msaliti, jina maarufu likawa msaliti mkuu Trotsky mpaka kitabu kiliandikwa kuchambua usaliti wa Trotsky kutokana na matakwa ya Stalin. Oktoba 23, 1926, ikiwa ni miaka miwili baada ya Lenin kufariki dunia, Stalin alitumia mamlaka yake kushawishi na kumfukuza Trotsky kwenye chama na kumuondoa kwenye vyeo vyote alivyokuwa navyo, ikiwemo ujumbe wa Baraza la Politburo maana kumuacha kwenye baraza la maamuzi ni kikwazo kwake. Kufatia uhasama huo Mwaka 1940, Trotsky aliuawa kwenye shambulio lenye utata na baadae Ikaja ikaaminika kuwa Stalin alihusika na mpango huo wa mauaji ya Trotsky, Stalin alifanya hivyo ili kujirahisishia njia yake ya kuongoza Dola ya Kisovieti bila vizingiti vyovyote.

Baada ya kuikamata nchi na kujihakikishia kuwa yeye ndie Urusi mara moja alianza kupenyeza mamlaka yake na kulijenga taifa la kisoviet katika dhana na nadharia zake, hatimae Urusi ikawa Stalin na Stalin ikawa Urusi.

Huyu Joseph Stalin aliyeigeuza dunia kuwa Urusi akipeperusha bendera nyekundu ya kijamaa dunia nzima alizaliwa Desemba 21, mwaka 1878 katika eneo la Gori nchini Georgia ambayo lilikuwa ni eneo la utawala wa kirusi, Stalin jina lake halisi alilopewa na wazazi wake wakati huo anazaliwa ni Losif Vissarionovich Dzhugashvili. Baba yake Stalin alikuwa na sifa ya ulevi wa kupindukia na aliyependa ugomvi mara kwa mara na kutokana na tabia yake hiyo akawa mbali na familia yake hivyo Stalin alilelewa na mama yake muda mwingi. Mwaka 1894 Stalin alipata nafasi ya kwenda seminari ya Tiflis Nchini Georgia wakati huo kukiwa na vuguvugu la mapinduzi.

Tofauti na matarajio ya familia yake, Stalin akiwa seminari badala ya kujikita kwenye masomo ya theolojia akatumbukia katika kundi la Marxi naye akawa Kiongozi wa siri wa kundi hilo katika tawi la Seminari ikumbukwe kuwa kipindi hicho kulikuwa na vuguvugu la mabadiliko na kuongezeka kwa nadharia ya ujamaa ambao ulichochea mapinduzi ya mwaka 1917. Hata hivyo jitihada zake zilibainika na uongozi wa shule na hivyo kufukuzwa seminari. Alifukuzwa akiwa katika harakati za kufanya mapinduzi .

Baada ya kukwama kwa jaribio lake la awali akaamua kusaka kazi ya ualimu na baadae karani katika ofisi, Pamoja na kazi hizo Stalin aliendelea kuwaza namna ya kuendesha mapinduzi. Ndipo alipoamua kupanga mbinu za mapinduzi nyakati za Usiku. Mwaka 1898 akajiunga na chama cha social Democratic Party cha Urusi. Miaka miwili baadae ,Stalin akapanga maandano ya wafanyakazi na migomo katika maeneo makuu ya viwanda maadamano ambayo hayakufanikiwa kutokana na ushiriki hafifu na hamasa ndogo kutoka kwenye chama hicho. Kufatia hatua hiyo Stalin alijivua chama hicho na mwaka 1903 akajiunga na chama cha Bolsheviks chama cha kijamaa kilicho kuwa na nadharia juu ya wafanyakazi na wakulima, Stalin ndani ya chama hicho aliteuliwa kuwa mtaalamu wa kupanga wizi na namna ya kupata fedha kwaajili ya kufadhili mapinduzi.

Ingawa baadae alikamatwa na kufungwa, Stalin alikuwa mwepesi wa kutoroka jela. Desemba mwaka 1905, alikwenda Finland kwa kuhudhuria mkutano wa chama chake. Huko akakutana na Lenin kwa mara ya kwanza. Miaka miwili baadae ,Stalin akasuka mipango ya kuvamia basi lililokuwa katika mji wa Tiflis .basi hilo lilikuwa limebeba fedha nyingi. Katika tukio hilo, watu 40 walifariki dunia na wengine 50 kujeruhiwa vibaya sana wakati basi hilo lilipovamiwa na kuporwa kiasi cha dola za marekani milioni 3.5.

Baada ya kufanikiwa kupora fedha hizo ,Lenin alivutiwa na werevu wa Stalin na inaripotiwa kuwa Lenin alitamka wazi kuwa "huyu ndiye mtu sahihi ninayemhitaji". Mwaka 1912 ,Lenin akamteua Stalin kuwa katika kamati kuu ya Bolsheviks na kumpa ujumbe wa bodi katika gazeti la chama la Pravda. Jina lake la awali alilopewa na wazazi wake la Losif Vissarionovich aliachana nalo rasmi mwaka 1913 na tangu wakati huo akajulikana kama Stalin ikiwa na maana ya "mtu wa chuma" mwaka huohuo alikamatwa na kupelekwa nchini Siberia alikosota hadi mwaka 1917.

Mwaka 1914 katika vita vya kwanza vya dunia alikuwa mmoja wa waliokuwa na uchu wa kupambana walishirikiana na ufaransa na uingereza. Kwa ujumla alifanya kazi kwa ukaribu sana na Lenin kwa kupanga mikakati mingi iliyokuwa na lengo la umwagaji damu Kwa kile walichoamini kuwa ni kwa ajili ya maslahi ya urusi. Kwa ushirikiano huo wakafanikiwa kufanya mapinduzi Novemba 6 1917, wakianza kuudhibiti mji wa saint Petersburg na baadae nchi nzima. Kutokana na mapinduzi hayo, Urusi ikajitoa vitani na Stalin akafanywa kuwa waziri katika utawala huo wa kikomunisti chini ya Lenin.

Lakini Stalin alikuwa mjanja sana kama nilivyo eleza huko juu Stalin ambae daima aliangalia mbele na mustakabali wake kutokana na hali hiyo alipanda vyeo ndani ya chama. lakini wakaja kusigana na Lenin kuhusu utawala ndani ya chama hasa baada ya Lenin kutoka mapumzikoni alikokuwa anaumwa ugonjwa wa moyo. Lenin alitangaza kufukuzwa kwa Stalin lakini kutokana na nguvu yake kuwa ndogo bila kujua kuwa tayali Stalin ameshajiimarisha ndani ya chama cha communist cha Bolsheviks Stalin akaendelea kuvuma katika nafasi yake ya ukatibu mkuu hadi Lenin alipoiaga dunia januari 21, mwaka 1924 na nafasi yake kuchukuliwa na Stalin.

Baada ya Stalin kuyatwaa madaraka Stalin akaja na mbinu mpya ya kuwapeleleza viongozi wenzake jambo ambalo alilifanya kwa uangalifu mkubwa huku akijiandaa kuwa dikteta na mtawala mwenye mamlaka makubwa ndani ya Soviet Union, baada ya kufanikisha mkakati huo akaja kuwa kiongozi aliyevuma ndani ya urusi lakini pia aliyetisha kwa matendo yake ya kudhibiti adui zake, alijipachika majina kibao ya sifa na mengine akipewa na wapambe wake, aliitwa "jua linalong'ara" "mwalimu bora na rafiki " "tumaini la walalahoi na wafanyakazip" na " mtu mwerevu aliyepata kutokea katika uso wa dunia".

Mwaka 1928 alitangaza mpango wa miaka mitano kwa urusi akisema kuwa taifa hilo lazima liharakishe maendeleo ili lisiangamie. Ndipo dunia ikashuhudia urusi ikiwa katika chati ya juu kiuchumi na ujenzi wa viwanda kwa kasi ya ajabu .lakini pia mipango mingine ilionekana wazi kuwa isingeweza kutekelezeka nje ya hapo aliijenga Urusi kuwa taifa la viwanda. Aliongoza katika mageuzi makubwa ya kiuchumi huku maendeleo na Uchumi wa Urusi uliimalika na kuwa dola lenye uchumi mkubwa duniani lenye ushawishi mkubwa na uwezo mkubwa wa siraha za nukria.

Hata hivyo Joseph Stalin alifariki dunia machi 5 mwaka 1953, baada ya kupooza akiwa nyumbani kwake, hata hivyo ,zipo habari kwamba Stalin alipewa sumu maalumu itakayo mfanya kupoza na baadae kufa ili kuzuia mpango wake wa kuanzisha vita ya nyuklia dhidi ya marekani, kufatia kifo chake maelfu walikusanyika jijini Moscow kushuhudia mwili wake wasiamini kama Stalin ameaga dunia. Kufatia kifo cha Stalin Georgy Malenkov akarithi nafasi yake.

Ukimtazama Stalin kwa upande huu unamuona kama kiogozi shupavu atakaye kumbukwa kwa mengi ndani ya umoja wa Soviet, ni Stalin na Ile ilikuwa Urusi kuu. Tukiachana na Stalin na Ile iliyokuwa dola la Kisoviet sasa tuitazame Urusi ya Putin, Vladimir Putin kiongozi ushupavu kama Stalin, Putin ni mbabe kama Staln mwenye kuyapenda madaraka lakin hakuyatafuta kwa nguvu kama Stalin, ndani ya Putin Stalin anaishi japo wanatofautiana njia za kuingia Ikulu ya Kremlin. Joseph Stalin aliyataka madaraka kwa nguvu zote huku Vladimirovich Putin alilazimishwa kuwa raisi kwa kuogopa kuwa Urusi ilikuwa na matatizo mengi, lakini leo hii hataki kuachia uraisi.... Ebu tumtazame Vladimir Vladimirovich Putin ni nani? Na Kwanini tuseme ndani yake Joseph Stalin anaishi?

Vladimir Vladimirovich Putin alizaliwa Oktoba 7, 1952 katika mji wa Leningrad katika Ile iliyokuwa muungano wa kisoviet kutoka kwa wazazi wake wawili yani baba yake Vladimir Spiridonovich Putin na mama yake aliyeitwa Maria Ivanovna Putina ambae mama yake anajulikani kwa jina lingine kama Shelomova. Putin alipata elimu yake kuanzia September 1, 1960 kwenye shule ya msingi iliyoitwa No 193 huko Baskov Lane na baadae kwenye chuo cha Leningrad state university aliposomea sheria na alihitimu elimu yake hapo chuoni mwaka 1975. Baadae alijiendeleza elimu yake mpaka ngazi ya uzamivu (PHD) katika sheria za kibiashara yani business law.

Mwaka 1975 Putin alijiunga na shilika la kijasusi la Urusi la KGB na alianza kupewa mafunzo yake kwenye kikosi namba 401 huko Okhta kwenye mji wa Leningrad, toka hapo alipitia ngazi nyingi ndani ya kikosi hicho cha kijasusi cha KBG. Kuanzia mwaka 1985 mpaka 1990 Putin alitumwa huko Ujerumani mashariki Kama afisa wa ngazi ya juu kwenye kikosi maalumu cha ujasusi cha KBG, baada ya ukuta wa Berlin kuanguka mapema tarehe 9,11,1989 na chama cha kikomnist cha Ujerumani mashariki kufutika alilejea Leningrad Urusi ambapo alipangiwa kufanya kazi za kijasusi kwenye Kitengo maalumu cha masuala ya kigeni mpaka alipo staafu mwenyewe akiwa na cheo cha lieutenant colonel August 20 1991.

Hivyo Vladmir Putin ni afisa wa kitengo cha ujasusi cha KGB aliyekuwa na cheo cha “Lieutenant Cornel” ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye majeshi ya Urusi yaliyokuwa nchini Ujerumani Mashariki; Putin ni mtu jasiri sana, anayejiamini na mwenye tabia ya kuchukuwa maamuzi magumu. Watu wengi wanaomjua Vladimir Putin kwa karibu wanakuambia kwamba Putin ana kila aina ya sifa ya ujasusi; ni mtu asiyetaka mizaha, wakati wote yupo serious na mtu wa majukumu wakati wote, Wengi wanakuambia ni vigumu kumuona Putin akicheka, anaweza akatabasamu, lakini tabasamu hilo haliwezi kudumu kwa zaidi ya swekunde tano.

Putin pia ni mtu mkakamavu sana na mwanamichezo mzuri anayeheshimika duniani kote kwa kuwa na mkanda mweusi (Black Belt) wa mchezo wa Judo na Karate; pia anapenda sana kukimbia na farasi na kucheza michezo mbalimbali inayohusiana na farasi. Putin pia ni rubani mzuri sana wa ndege za kijeshi, mwaka 2001 alichukuwa ndege ya kivita akiwa peke yake kama rubani na kwenda kushambulia Chechnya na kurudi salama. Putin ana kawaida yake akitembelea nchi yoyote ambayo mchezo wa Judo una wapiganaji, basi lazima kwanza kabla hajafanya lolote katika nchi hiyo ya ugenini ni lazima apambane na bingwa wa mchezo huo wa uzito wake na lazima ampige; katika historia yake hajawahi kupigwa na mpinzani wake hata mara moja. Putin ni mtu anayeipenda sana nchi yake (Nationalist), ni mtu anyeamini kwamba hakuna taifa bora duniani kama Urusi na hakuna watu bora na mila bora duniani kama Warusi na mila zao.

Vladmir Putin ni mjukuu wa mpishi wa kiongozi wa zamani wa kikomunist Vladmir Ilichy Lenin, Babu yake Putin aliyeitwa Vladimirovich Spiridonovich Putin alikuwa mpishi mkuu wa Vladimir Lenin kwa miaka yote ya utumishi wake na hata Vladimir Putin kujiunga na kitengo cha ujasusi cha KGB inatokana babu yake kuwa karibu sana na utawala wa kikomunist. Baada ya kuvunjika kwa umoja wa Soviet Union mwaka 1991 na Ukuta wa Berlin kuvunjwa, Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi ziliungana na hivyo majeshi ya Urusi yaliyokuwa yanaulinda ukuta wa Berlin walirudi nyumbani ikiwa ni pamoja na kikosi chote cha KGB, kutoka kwenye kazi ya ukachero kwenye kitengo cha KGB Putin aliingia kwenye siasa chini ya utawala wa Boris Yelstin na kuwa waziri wa wizara mbalimbali kabla hajaombwa mara kadhaa kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo na bosi wake, lakini kila alipoombwa alikataa na kusema Russia ina matatizo mengi hataweza kuyatatua. Kwa sasa rais Vladimir Putin ametengana na mke wake wa miaka mingi Lyudmila Putina, na kwa hivi sasa anaishi na msichana mdogo mwenye umri wa miaka 20 Putin anaongea na kuandika lugha ya Kijerumani kwa ufasaha wa hali ya juu.

Pamoja na kwamba rais Vladimir Vladimirovich Putin amekuwa rais wa Urusi kwa vipindi viwili tofauti, na leo hii na anadaiwa kuwa kiongozi makini wa taifa hilo, lakini hakuna mtu yeyote aliyekuwa akimtegemea kwamba siku moja angelikuwa rais wa taifa hilo kubwa duniani, hata yeye mwenyewe alikuwa hatarajii kwamba siku moja atakuja kuwa rais wa Urusi kwa vile alikuwa anaugopa sana urais. Putin aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Serikali ya rais wa kwanza wa Russia Federation Boris Nikolayevich Yelstin.

Wakati rais Boris Yelstin amechoka kutokana na maradhi ya moyo na umri wake kuwa mkubwa alimtafuta mrithi wake kwa muda mrefu bila ya kumpata, aliwahi kumuita Putin mara mbili ofisini kwake kwa nyakati tofauti katika vipindi visivyopungua miaka miwili akimtaka yeye awe ndiye mrithi wake wa kiti hicho cha urais, lakini Putin alikataa kata kata akisema haiwezi kazi hiyo labda amtafute mtu mwingine. Tofauti ya Putin na Stalin ni hiyo, Stalin aliye utafuta urais kwa nguvu na tamaa ya hali ya juu lakini huku Putin akionekana kuukimbia uraisi.

Rais Boris Yelstin aliendelea kumtafuta mrithi wake miongoni mwa mawaziri wake na hata viongozi wengine wa idara zingine za Serikali bila ya mafanikio, na baada ya miaka miwili kupita alimuita tena Putin ofisini kwake, na huku akimsihi kwamba ameangalia nchi nzima, lakini haoni mtu mwenye uwezo wa kumuachia nchi zaidi ya yeye (Putin), Putin wakati huo akiwa kama waziri tu wa wizara alimkatalia tena kata kata kwa mara ya pili kwamba kazi hiyo haiwezi labda atafute mtu mwingine. Putin aliondoka na huku akimwacha rais wake Boris Yelstin akipasua kichwa kuhusu nani wa kumkabidhi madaraka ya urais

Baada ya miezi sita kupita rais Boris Yelstin akiwa amebakiza muda wa miaka miwili amalize muda wake wa kuwa rais kikatiba alimuita Putin ofisini kwake, na Putin alipoingia ofisini kwake (rais) alimpisha kiti Putin akae, Putin alikataa kukaa, rais Boris Yelstin alimshika mkono na kumlazimisha kukaa kwenye kiti chake (kiti cha rais) Putin alipokaa akamuambia wewe sasa ndiyo rais wa Russia Federation kuanzia leo hii, na kama hutaki ondoka kwenye kiti nchi ibakie bila kuwa na mtawala Putin aliendelea kuwa rais kwa wiki moja bila ya wananchi kufahamu wakati huo rais Boris Yelstin alikuwa akimumkabidhi documents muhimu za ofisi na baada ya wiki moja akampeleka bungeni kumtambulisha rasmi kwa wabunge kwamba Russia Federation imepata rais mpya na yeye anang’atuka kwa sababu za uzee na maradhi ya ugonjwa wa moyo yaliyokuwa yanasumbua mara kwa mara, ikumbukwe Boris Yelstin alipata “Heart Attack” mara mbili kabla ya kumkabidhi kiti Vladimir Putin.

Putin akaanza kazi kama rais asiyekuwa na uzoefu na huku baadhi ya wanasiasa wengine wakiwa na hofu kwamba kazi ya urais itamshinda. Rais Putin alianza kwanza kuisafisha Ikulu ya (Kremlin) kwa kumfukuza kazi mtoto wa rais mstaafu Boris Yesltin Tatiana ambaye alikuwa na maskendo mengi ya ufisadi kwenye ofisi ya rais, Tatiana Yelstin wakati baba yake akiwa rais yeye alikuwa msaidizi wake na Tatiana huyo huyo alikuwa rafiki wa karibu wa mahusiano ya kimapenzi na Professor Berozosky ambaye alikuwa mshauri wa mambo ya usalama wa rais Yelstin.

Professor Berozosky alikuwa Mrusi mwenye asili ya Kiyahudi (kabla ya kujiunga na siasa alikuwa Professor wa Hesabu wa Moscow State University “MGU”), Professor Berozosky ni binamu zake Roman Abrahamovich (Billionea wa Chelsea) na Mikhael Khadarakovsky (Aliyekuwa billionea mkubwa Urusi na kufungwa maisha na Putin kwa kupatikana na hatia ya mauwaji) wote hawa wawili ni mabinamu wa Professor Berozosky na walipewa ubillionea na binamu yao kwa kukabidhiwa visima vya mafuta kwa utaratibu mbovu wa ubinafsishaji, kwa vile Professor Berozosky alikuwa mshauri mkuu wa rais na pia alikuwa na mahusiano ya karibu na mtoto wa rais.

Utajiri wa Professor Berozosky unakadiriwa kuwa Pound za Uingereza 26 Billions, wakati utajiri wa Roman Abrahamovich unakadiriwa kuwa US $ 12 billion,na Mikhael Khadarakovsky unakadiriwa kuwa US $ 16 Billions. Ikumbukwe kwamba Russia ina mabilionea zaidi ya 200 na zaidi ya mabilionea 100 ni Warusi wenye asili ya Kiyahudi ambao wote hawa waliwezeshwa na Myahudi mwezao alipokuwa Ikulu Professor Berozosky.

Putin alipoingia madarakani kama rais wa Russia kwa kipindi cha mpito cha miaka miwili, jambo la kwanza alilolifanya ilikuwa ni kuwafukuza kazi Tatiana Boris Yelstin na Professor Berozosky, jambo ambalo halikumfurahisha Professor Berozosky na baada ya hapo alianza malumbano na Putin, wakati Putin anapanga kumkamata na kumfungulia mashitaka ya ufisadi Professor Berozosky, alibonyezwa na watu wake wa karibu hivyo kabla hajakamatwa alikimbilia nchini Uingereza ambapo alikuwa adui wa Serikali ya Urusi hadi alipokufa kifo cha kutatanisha huko nchini Uingereza.

Putin ameongoza vipindi viwili kama rais na kipindi kimoja kama waziri mkuu na hivi sasa ni rais tena kwa kipindi cha tatu kama rais, na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wa Urusi wanakuambia kwamba Putin anatamani awe rais wa maisha wa nchi hiyo ikumbukwe cheo hicho cha urais aliitwa mara tatu ili akabidhiwe nchi, lakini alikikataa na kusema kazi hiyo haiwezi, leo hii hataki hata kuondoka.

Uamuzi wa Putin kuingiza Majeshi yake Cremia, Ukraine yanatokana na misingi ya kihistoria kwakua historia ya kisiwa cha Crimea ambacho kipo kusini mashariki mwa Ukraine ilikuwa ni mali ya Russia federation, kisiwa hiki hadi mwaka 1954 kilikuwa ni kisiwa cha Russia Federation, lakini mwaka huo wa 1954 Nikita Khrishov raia wa Ukraine ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama cha kikomunist cha Soviet Union na ambaye pia alikuwa kiongozi wa Soviet Union aliizawadia Ukraine kisiwa hicho cha Crimea kutoka Russia Federation.

Mwaka 1991 baada ya jumuiya ya Soviet Union kusambaratika kulikuwepo na makubaliano kati ya Russia Federation na jumuiya ya kimataifa kwamba silaha zote za Nuclear zilizokuwa zikimilikiwa na Ex-Soviet Union zikabidhiwe kwa Russia Federation ikiwa ni pamoja na meli za kivita na kituo cha kivita kilichoko kwenye kisiwa cha Crimea, na kwa upande mwingine Russia na Ukraine walikubaliana kwamba Ukraine isijejiunga na European Union na kuruhusu majeshi ya NATO kuweka kituo cha kivita kwenye kisiwa hicho cha Crimea. Hivyo kitendo cha Ukraine kuwa na mipango ya kujiunga na European Union ni kukaribisha majeshi ya NATO kuja na kuweka kambi ya kijeshi Crimea, kisiwa ambacho kipo mpakani kati ya Ukraine na Russia ndio chanzo cha vuta nikuvute baina ya Ukraine na Russia. Hiyo ndiyo sababu kubwa inayomfanya rais Putin wa Russia kuwa na ujasiri wa kukivamia kisiwa hicho ambacho asilimia kubwa ya wakazi wa kisiwa hicho ni Warusi na lugha inayotumika huko ni Kirusi zaidi kuliko Kiukraine.

Putin raisi wa zama hizi ndani ya Urusi ni mtu anayetajwa kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha yani mtu tajiri wa kuogopwa, lakini kwa taarifa iliyotolewa na tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Urusi imeeleza kuwa, Rais Putin alijipatia mapato ya Rouble Milioni 38.5 za Urusi sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 1.9 kati ya mwaka 2011 na 2016. Hiyo maana yake ni kwamba kiongozi huyo wa nchi ya Urusi ana mshahara wa Dola za Kimarekani 143,000 kwa mwaka. Fedha hizo hazizidi hata theluthi moja ya ule anaopokea Waziri Mkuu wa Australia, Malcom Turnbull ambaye hulipwa Dola za Kimarekani 527,852.

Kwa mujibu wa Gazeti la Washington Post, Rais Putin pia ameorodhesha akaunti 13 za benki mbalimbali ambazo kwa pamoja zina akiba ya Dola za Kimarekani 307,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 650. Rais Putin pia ameorodhesha kumiliki nyumba zake mjini St Petersburg, hisa katika benki moja pamoja na magari mawili ya kimichezo ya nyakati za uliokuwa Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR). Ingawa mshahara wa Rais Putin unaweza kuwa mdogo ikilinganishwa na viongozi wengine duniani, ni mkubwa mno ikilinganishwa na wanaopata raia wa Urusi. Raia wa Urusi kwa wastani hupata Dola za Kimarekani 8500 kwa mwaka nao hupata watu wachache.

Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti hivi karibuni kuwa Rais Putin alitakiwa kutoa takwimu za kipato chake na mali alizonazo kama sehemu ya mchakato wa usajili kwa wagombea urais kutokana na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 18 mwaka huu. Taarifa hizo zimekuja huku wakosoaji wake wakidai kwamba Rais Putin ana utajiri wa kupindukia na wakimuweka daraja moja na hata zaidi ya matajiri mabilionea wa dunia.

Ratiba ya kila siku ya Vladimir Putin ina mambo mengi zikiwemo saa kadhaa za kuogelea, kuchelewa kulala, kutokunywa pombe kabisa. Unapotaka kumfurahisha Rais wa Urusi, Vladimir Putin, mpatie vitu viwili, mbwa mtukutu kabisa na kifungua kinywa cha mayai ya ndege wa porini aina ya tombo. Jarida la Newsweek la Marekani limeripoti kuwa vitu hivyo vinapatikana kutoka “mashamba ya rafiki yake ambaye ni kiongozi wa dini nchini Urusi anayeitwa Kirill.

Hiyo ni kwa mujibu wa wasifu wa Putin ulioandikwa mwaka 2014 na mwandishi wa jarida la Newsweek, Ben Judah aliyetumia miaka mitatu kumfanyia utafiti Rais huyo wa Urusi kwa ajili ya kitabu chake kinachoitwa, “Fragile Empire: How Russia Fell in and Out of Love with Vladimir Putin.”

Rais huyu wa Urusi hivi karibuni amekuwa akitajwa nchini Marekani kwa mambo mbalimbali ikiwamo kufanya utafiti unaolenga kubaini kampeni za Rais wa Marekani Donald Trump, msimamo wake juu ya mgogoro nchini Syria na alichokiongea kuhusu Marekani kujitoa katika majadiliano ya hali ya hewa nchini Ufaransa. Putin amekuwa akishinda uchaguzi zote za rais anazo shiriki toka Ile ya mwaka 2000 na ya mwaka 2004 ambayo alichaguliwa upya na kushinda, hivyo kuendelea na kipindi chake cha pili hadi Mei 7, 2008 kabla ya kuachia utawala wa nchi kwa Damitry Medvedev aliyeshinda kiti cha urais. Medvedev nae kwa kutambua umuhimu wa Putin, mara moja alimteua kuwa Waziri Mkuu katika kile kilichoelezwa kuongoza kwa pamoja bila kinyongo (tandemocracy).

Jina Putin lina asili ya watu wa mashariki mwa Urusi likiwa na maana ya mila katika mji wa Leningrad alikozaliwa.


Email- mbwanaallyamtu990@Gmail.com
IMG_20190507_100215_704.jpeg
 
Me napenda hiyo stly yao ya kuongoza kat ya putin na Damitry
 
Historia inavutia tukipata raisi anayefanana na Putin tutapiga hatua ndefu ndefu.
 
Kuna mmoja huku na yeye alisema alikuwa anabipu tu ila ikapokelewa (alisukumizwa). Alisema anatamani hata leo akapumzike! Sasa hataki kutoka anasema nani ataendeleza mamiradi ya barabara, umeme na mandege! Madaraka matamu sana.
 
Mkuu, acha uongo wa kitoto..

Boris anavyojiuzuru Putini alikuwa waziri mkuu, kwa katiba ya urusi ,ikitokea Rais akajiuzuru/akafariki, waziri mkuu hurithi nafasi ile ya urais mpaka uchaguzi..

Sasa unapo ongopa eti akampa nchi bila wananchi kujua alafu akampeleka bungeni na kumtambulisha unakuwa unawadanganya wajinga..
 
Back
Top Bottom