Russia inadai vikwazo lazima viondolewe kabla ya usitishaji vita wa baharini wa Ukraine kuanza

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
17,999
Reaction score
21,560
Tofauti na baadhi ya watu walivyokuwa wakidai kwamba Russia walikuwa hawaathiriki na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na mataifa ya magharibi lakini sasa ukweli umedhihirika kwamba Russia inaumizwa sana na hivyo vikwazo.

Russia imesema baadhi ya vikwazo vya nchi za Magharibi lazima viondolewe kabla ya kuanza usitishaji vita wa baharini na Ukraine.

Ndani ya saa chache baada ya Marekani kutangaza kuwa pande hizo mbili zimekubali kusitisha mgomo katika Bahari Nyeusi katika mikataba tofauti, Ikulu ya Kremlin ilisema itafanyika mara tu vikwazo kwa benki kadhaa za Russia vitakapoondolewa.

Madai hayo ni pamoja na kubatilisha vikwazo kwa benki ya serikali ya kilimo ya Rosselkhozbank na kurejesha ufikiaji wa makampuni kwenye mfumo wa malipo wa kimataifa wa Swift.

Usiku kucha, Moscow ilizindua shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye mji wa bandari wa Mykolaiv, maafisa wa Ukraine walisema, huku Rais Volodymyr Zelensky akisema kuwa mashambulizi hayo ni "ishara ya wazi" Russia haitaki amani.

 
Ilimradi urusi awe kashindwa
 
Russian wako very smart!
Wapatanishi wanamuuliza Ukraine masharti yako ili vita visitishwe ni yapi? Mukraine anachagua maeneo yanayo mtesa yasipigwe kama vigezo! Mrussia anapata mojamoja habari za kijasusi za kivita kuwa kumbe huyu hapa ndio pana mbana! Naye anatoa vigezo ambavyo anajua havitakubalika kirahisi na anaanza kupiga kwenye mshono!! Kiufupi hii vita haitaisha mpaka russia ametimiza lengo!
 
Kumbe vikwazo vina muathiri? Basi waongeze dozi hapo hapo mpaka anyooke.

Kaishiwa risasi anaomba kwa Kim, kweli simba akizidiwa hula majani.

Huu ndio muda wa kumtandika kama katoto sasa.
 
Umehama mada sasa sijui ni kwa uelewa mdogo au ni kwa ushabiki maandazi tu. I just don't know.
 
Mimi nataka hii vita isiishe ili trump asipate sifa imehenteshe mpaka akome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…