Maafisa wa Kremlin wanahatarisha matarajio ya uwekezaji wa faida kubwa kwa makampuni ya nishati ya Marekani, inaonekana wanataka kumshawishi Rais Trump kwamba mafanikio makubwa ya kiuchumi yanaweza kuja kutoka kwa Moscow katika kumaliza vita vya Ukraine na kufuta vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Russia.
Hakuna shaka kuwa Russia ina hazina kubwa ya mafuta na gesi asilia, lakini juhudi za kuyavutia makampuni ya nishati ya Marekani au mataifa mengine ya Magharibi kutekeleza miradi ya Russia huenda yakakumbana na mashaka, si haba kwa sababu ya historia ya hivi majuzi ya kampuni hizo nchini Russia.
Hata hivyo, Kirill Dmitriev, afisa wa fedha wa Kremlin, alionyesha matumaini wiki iliyopita kuhusu matarajio hayo, akiweka uwezekano wa fursa za uwekezaji na makampuni ya Magharibi, ikiwa ni pamoja na wazalishaji wa mafuta.
Makampuni ya nishati yangehitaji kupima upatikanaji wa mafuta na gesi asilia dhidi ya hatari zinazoweza kutokea, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa sifa kutokana na kushiriki katika sekta ambayo imeendeleza kifedha serikali inayopigana vita dhidi ya jirani yake.