Russia World Cup 2018: France crowned World Champions after defeating Croatia 4-2

Refa wa jana alinifurahisha sana sana dah ilikuwa imebakia kidogo tu amtandike makofi Neymar
 
Hakuna cha samba wala umaza wala udada..kazi kazi tu na ndiyo ubelgiji alivyowafanya hawa nguruwe 😀😀😀😀
Hahaha!! Usiwe umeendeleza chuki kwa Brazil kisa Neymar wa Barcelona.

Belgium walitumia nafasi vizuri,Brazil walipata nasafi nyingi.

Neymar world cup hii kwa upande wangu kachemka sana alikuwa anajilegeza sana kama mtu asiye pata mlo kamili wakati mwingine nikawaza au majeruhi yaliyompata mwezi February,.

Aisee sasa naona Cr7 na Mess bado wananafasi hata ya miaka mitatu kutawala soka.

Wiliian sijui anamatatizo ya familia au kisaikolojia toka world cup imeanza skuwa na imani naye si yule wa chelsea.

World cup hii inasurprise za kutoshaa
 
Wee acha tu mkuu, ni majanga
Kabisa,wachaa tutazame waliosalia.

Bwana mdogo Neymar itabidi aingiee gym naona hana nguvu za mwili na kujilegeza kizembe sana.

Neymar hii world cup kaniangusha sana,uchezaji wake abadilike katika utoaji pasi wa haraka na aache kujilegeza ...kufikia level za Cr7 au messi bado anashughuli nzito.

Kipindi cha pili walau tuliiona samba Brazil.
 
Mkuu kuhusu Neymar jiba ni rahisi tu Media zinamkuza sana kuliko uwezo wake uwanjani huu mpira anaocheza Neymar Leo Ronaldo alicheza Manchester United 2007 yeye anaocheza Leo akiwa na miaka 26
 
Ni kweli mkuu Neymar mpaka nahisi anakua overated kwasababu za kibiashara lakini hjafikia level za kina CR7 na Messi

Pia ili Brazil ifanye vizuri hasa katika umaliziaji lazima wawe na namba tisa wa asili kama walivyokua kina Romario na Ronaldo de Lima, hapo ndio falsafa ya Samba itafanya kazi sawasawa vinginevyo watakua wanafanya vizuri katika mechi ambazo hazina pressure lakini kwenye serious encounters na serious contenders siku zote watakua wanachemsha
 
Umeeleza vyema sana,

Sasa kupata namba tisa kama za Ronaldo de lima ni shughuli kweli kweli.

Wajipange upya 2022,walau hii ndio ilikuwa nafasi nzuri kwa wachezaji waliokuwa nao kipindi hiki.
 

Hahaaa hapana kiongozi sina chukinae unless anaikosti timu,, muda mwingi anakaa na mpira alafu mchoyo wa pasi.
 
Mkuu kuhusu Neymar jiba ni rahisi tu Media zinamkuza sana kuliko uwezo wake uwanjani huu mpira anaocheza Neymar Leo Ronaldo alicheza Manchester United 2007 yeye anaocheza Leo akiwa na miaka 26
Ndio ndio umezungumza vyema,
Cr7 kipindi yupo Manchester united alicheza sana mpira kama huu wa neymar mpaka ikafika kipindi Jose mourinho kipindi yupo Chelsea akawa anamponda kwamba anajiligeza sana na anabebwa na marefarii.

Baada ya kuondoka man u kwenda real Madrid jamaa alibadilika sana uchezaji wake akawa yeye na goli goli na yeye ikawa ni mashine ya kuzalisha mabao,unaweza maliza hata mechi tano hujamuona Ronaldo akifanya mbwembwe au vyenga vya madaha kama old Trafford,kwakweli jamaa alifanya mabadiliko chanya na yenye afya.

Cr7 huyu jamaa anafanya mazoezi ya kutisha kunakipindi flani nilikuwa na picha zake mwanzoni akiwa real Madrid gym ilikuwa imeiva imeshika mkono haswahaswa,na naamini mpaka sasa bado namuona ananafasi kubwa ya kusumbua watu.

Mimi huwa ni muumini wa burudani na goli kama Gaucho hivyo niliona Neymar anaweza kuvaa viatu vyake kiukweli bado aniniangusha lakini bado nampa muda.
 
Hahaaa hapana kiongozi sina chukinae unless anaikosti timu,, muda mwingi anakaa na mpira alafu mchoyo wa pasi.
Kwa kweli hili la kukaa na mpira muda mwingi alifanyie kazi,

Lakini Mimi naamini huwa anakaa na mpira kwa muda ili afanye mbwembwe zake na madoido.

Inabidi aweanatazama si kila mechi ni ya kufanya madoido mechi zingine inabidi kutupilia mbali utundu wa kuchezea mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…