Russia World Cup 2018: France crowned World Champions after defeating Croatia 4-2

Nafukua makaburi
ahsante sana MUNGU.
nilifikiri spain wamepata dawa ya kupambana na timu zinachocheza soka la kujihami kumbe badoooooo
22 MAY pia niliandika maneno yafuatayo baada ya kikosi cha hispania kutangazwa:


  1. mashabiki wa hispania musijifanye ya kwamba mumelisahau tukio hili lililotokezea 13/06/2014 kwenye nchi ya brazil na bahati mbaya baada ya kushitakiwa kwa kosa la shambulio la aibu matokeo ya mechi hii nimeshayasahau ila nakumbuka spain alishinda magoli matano (natania)
  2. nawakumbusha ya kwamba kabla kombe la dunia halijaanza benchi la ufundi la hispania linapaswa liwe limeshaandaa plan B ya kupambana na timu ambazo zimeshafahamu mfumo wao la si hivyo wajiandae kukutana na dhoruba kama ya mwaka 2014 nchini brazil
  3. wakati spain inakwenda kombe la dunia mwaka 2010 david villa na pedro rodriguez kwa pamoja walifunga wastani wa magoli 45 kwenye timu zao kama sijakosea, wakati huo david villa anachezea valencia na pedro rodriguez ilikuwa ni msimu wake wa pili tokea apandishwe kutoka la masia na josep guardiola. Iago Aspas na rodrigo moreno kwa pamoja msimu huu wamefunga magoli 41 ila bado siamini kama wanaweza kuvaa viatu vya fundi david villa ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa spain
  4. kwenye kombe la euro 2008 nakumbuka mzee luis aragones suarez alitengeneza utatu mtakatifu kwenye eneo la kiungo ambapo alikuwa anawatumia viungo marco senna ambaye alikuwa on fire licha ya majeruhi ya mara kwa mara, xavi hernandez akiwa kwenye ubora wake baada ya kufichwa kwa muda mrefu na deco souza pamoja na kiungo andres iniesta ambaye naye alianza kuuonyesha ulimwengu uwezo wake halisi wa mpira, kilichotokezea kimebaki kuwa ni historia yenye kuvutia.
  5. baadae (2010 na 2012) chini ya vicente del bosque anaamua kuwapa majukumu ya ulinzi viungo wawili ambao ni segio bosquet na xabi alonso ili kuifanya timu iwe na muunganiko kwenye eneo la ulinzi na ushambuliaji, baadae pia aliamua kuwapa uhuru mtu na ndugu yake (xavi na iniesta) ambao waliufanya mpira uonekano mchezo rahisi kwa watazamaji wanaoshabikia spain na pia waliufanya mpira uwe mgumu kwa timu pinzani.
  6. na kwenye eneo la ushambuliaji spain walikuwa wanacheza bila ya mshambuliaji anayesimama kwa adui ambapo alikuwa akimtumia david villa kama kiungo wa pembeni pamoja na david silva, kwa ufupi alichokifanya del bosque ni kucopy nusu ya mfumo wa guardiola akiwa barcelona na kilichotokezea kwa wapinzani aulizwe buffon na italy yake kwenye fainali ya euro 2012. ila kocha huyu wa sasa anachofanana na aragonez ni kwamba yeye pia anaamini mfumo wa kusimamisha strike wa uhakika kwenye eneo la adui na bila shaka atamtumia diego costa ambaye licha ya ubora hupata tabu sana kwenye total football.
  7. mfumo huu ni mzuri sana unapocheza na timu yenye viungo wabovu kama Argentina lakini ni mfumo hatari sana unapocheza na timu yenye viungo wenye uwezo wa kulinda na kushambulia kama Ufaransa na Ujerumani. Thiago Alcantara, koke, david silva,isco,iniesta na saul wote hawa ni viungo wanaopaswa kulindwa na mwanadamu mwenye nidhamu ya hali ya juu ndipo watakapoweza kuufaidi mpira wao lakini bahati mbaya Spain amebaki mwanadamu mmoja tu mwenye nidhamu kubwa kwenye kulinda ila bahati mbaya sana hajawahi kuonekana ni mchezaji muhimu kwa taifa lake, namkusudia JAVI MARTINEZ, wasipokuwa makini watamaliza kombe la dunia wakiwa wameruhusu magoli mengi kutokana na timu yao kukosa balance kwenye ulinzi.
 
Cesc Fabregas, Marcos Alonso and Alvaro Morata...come here, lets laugh on our way to Cobham[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
-Captain Cesar Azipilicueta
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Hii ni beti ya kitakatifu sio ya kusaka mpunga
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…