Waziri mkuu Mikhali Mishustin akiongea na raisi Putin kupitia video conference. Picha na TASS
Waziri mkuu wa Russia bwana Mikhail Mishstin mejitenga mwenyewe na shughuli zote zinazohusu mikutano na mikusanyiko baada ya kuambukizwa ugonjwa wa virusi vya COVID -19
Tayari bwana Mishustin anafuata maelekezo ya madaktari na alikwishamtaarifu rais Putin juu ya hali yake hiyo mapema Alhamisi ilopita na naibu waziri mkuu bwana Andrei Belouson ndie atakaimu nafasi yake.
Bwana Mishustin ambe ana umri wa miaka 54 aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa Russia tarehe 20 mwezi January baada ya raisi Putin kuleta jina lake licha ya majina mengine manne kupendkezwa na washauri wake.
Kuteuliwa na kisha kupendekezwa kwa jina la Mishustin kwa bunge la Russia liitwalo Duma kulikuja baada ya aliekuwa waziri mkuu bwana Dmitry Medvedev kujiuzulu nafasi hiyo.
Bwana Medvedev alijiuzulu yeye pamoja na baraza lake lote la mawaziri, ili kumpa nafasi raisi Putin kufanya mabadiliko ya kikatiba ambayo yalilenga kuondoa baadhi ya maamuzi ya kimamlaka kwa raisi.
Kitendo hichi kilimfanya raisi Putin aweze kupendekeza jina la Mishustin licha ya kuletewa majina manne ambapo jina la Mishustin halikuwemo.
Hivyo raisi Putin akapendekza jina la Mishustin kwenye bunge la Russia na bunge likampitisha Mishstin kuwa waziri mkuu wa Russia.
Mishustin ni mrusi ambae baba yake ana asili ya kiyahudi wa kutokea nchini Belarusi na kitaaluma ni mhandisi lakini pia mwenye ujuzi katika masuala ya uchumi na amefanya kazi mbalimbali zinazohusiana na uchumi.
Bwana Mishustin ameongoza mamlaka ya mapato ya Russia ijulikanayo kama FTS na kwa kipindi alichokaa hapo ameiwezesha idara hiyo kuweka taratibu nzuri za ukusanyaji wa mapato kubwa ikiwa ni kuhakikisha kila raia anajulikana kipato chake.
Pia ameifanya FTS kufanya shughuli za kijasusi zaidi kwa kuweka programs ambazo zinachunguza shughuli zote za kiuchumi nchi nzima ikiwemo kukusanya taarifa zote hususan zile zinazohusu miamala ya fedha kwenye mabenki na maduka ya fedha.
Pia ameiwezesha FTS kuweza kuona miamala ya fedha kwa wakati huohuo yaani real-time transaction na ni lazima wafanya biashara kama maduka kuingiza taarifa au data kwenye mfumo uitwao online cash register proxess.
Mifumo hii imewezesha pia kutambua watu wanekwepa kodi kwa kupitia mfumo wa kopyuta uitwao Artificial Intelligence.
Kama haitoshi bwana Mishustin pia amewezesha kutengenezwa kanzidata inayoangalia mapato ya kila raia yaani electronic income database.
Bwana Mishustin amekuwa wazri mkuu wa kwanza wa Russia kuweza kuchagua baraza lake mwenywe la mawaziri na viongozi wengine ambao wengi ametoka naeo idara ya FTS.
Hali hiyo haikuwahi kutokea huko nyuma na hali hii imepelekea kwa wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa kuwa huenda hii ni ishara kwamba bwana Mishustin anaandaliwa kuwa raisi wa Russia.
Jambo jingine kubwa la kuangalia ni kwamba inaonyesha wazi kwamba bwana Mishustin anapendwa na raia wa Russia kwa mtindo wa utawala wake tangia ateuliwe mwezi January.
Tangu aanze kazi amekuwa akizunguka nchi humoi kutembelea majimbo kadhaa na mwishoni mwa mwezi january aliagiza kuandaliwa makao makuu ya kushughulikia ugonjwa wa COVID-19.
Pamoja na shughuli zingine kufungwa katika kipindi cha ugonjwa huu pia nwaba Mishustin aliagiza wizara ya mawasiliano kuhakikisha kila mgonjwa wa COVID-19 nchini humo anafuatiliwa endapo anakiuka masharti ya karantini.
Katika mfumo huo mgonjwa ambae amevunja masharti hayo atapokea ujumbe mfupi wa simiu kuonywa juu ya tabia ya hiyo na endapo anaendelea kuvunja masharti hayo basi taarifa hupelekwa polisi ambao wanamshhughulikia mgonjwa huyo kwa muda wao.
Siasa za Russia zimekuwa ngumu kuzielewa katika miaka ishirini ilopita na ni raisi Putin na bwana Medvedev ndo ambao wamekuwa wakitawala nchi hii kwa muda sasa.
Kati ya nwaka 2008 na 2012 bwana Medvedev aliwa raisi wa Russia huku Vladmir Putin akiwa waziri mkuu wake.
Kati ya mwaka 2012 hadi mwaka 2018 bwana Medvedev akawa waziri mkuu huku Vladmir Putin akiwa raisi.
Hivyo mabadiliko yalofanywa mapema mwaka huu ni ishara tosha kwamba bwana Medvedev huenda akapendkezwa kuwa raisi wa Russia kwa kipindi kingine au wakabadilishana na bwana Mikhail Mishustin.
Lakini kwa jinsi rekodi ya Mishustin inavyoendelea kupaa juu, hiyo ni ishara tosha kwamba huyu ndie raisi ajae wa Russia.