1.Newton's First Law of Motion states that "An object at rest will remain at rest, and an object in motion will remain in motion unless external force is applied on it" (forbes. com by Abdo Riani).
Tafsiri yake katika lugha ya kiswahili ni kwamba "Kitu chochote Kilichokua katika hali ya utulivu kitaendelea kua katika hali hiyo hiyo ya utulivu, na kitu chochote kilicho katika hali ya mwendo kitaendelea kua katika hali hiyo hiyo ya mwendo isipokua hali hizo zitabadilika endapo nguvu kutoka nje itatumika.
Mfano; jiwe lililotulia tu mahali litaendelea kutulia hapo hapo labda kitokee kitu kitakacho lihamisha jiwe hilo kitu hicho chaweza kua nguvu ya maji upepo matetemeko ya arthi na hata binadamu kupitia shughuli zake. Pia vivyo hivyo kwa gari lililo kwenye mwendo litaendelea kua kwenye mwendo isipokua litaweza kusimama endapo tu kutakua na nguvu kutoka nje yakulizuia nguvu inaweza kua dereva amefunga breki mafuta yamekwisha ama limekwama katika kizuizi chochote kile.
Kwahiyo kupitia kanuni hii tunapata kutambua kua nguvu kutoka nje ndio mbinu pekee itakayotuamsha kama taifa na kua hai kutoka katika hali hii duni ya kimaendeleo tuliyonayo miaka nenda rudi (STATASI KUO).
Unaweza ukajiuliza kwani wenzetu waliwezaje(wazungu)? Ukweli ni kwamba mataifa yote yaliyofanikiwa duniani hapa tokea mwanzo mpaka sasa kwa namna moja ama nyingine wametumia kanuni hii, kivipi ni hivi mataifa ya ulaya yalikuwa yanawatu makini na wenye uwezo mkubwa kifikra (Akili) ila changamoto ikawa hawana rasilimali za kutosha kuweza kutosheleza mahitaji ya viwanda walivyo vianzisha hivyo ikawabidi watafute nguvu(rasilimali) kutoka nje ili kuweza kuendeleza shughuli za uzalishaji na maendeleo nchini mwao ndipo wakaja Afrika, Amerika na Asia kututawala(ukoloni),