Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Wajumbe wa chama cha UDA wamemuidhinisha Naibu Rais William Ruto kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya, utakaofanyika tarehe tisa mwezi Agosti mwaka huu.
Ruto sasa atamenyana na kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga kwenye uchaguzi mkuu.
Ruto alipokewa na mkewe Rachel pamoja na maafisa wakuu wa chama cha UDA mwendo wa saa tano kasorobo katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani, uliokuwa na yamkini wajumbe 5000 waliokuwa na mavazi ya manjano na kijani.
Baadaye aliidhinishwa na wajumbe 4,350 wa UDA bila ya kupingwa kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, kwenye hafla iliyofanyika faraghani.
Kiunzi cha pili cha Ruto sasa baada ya kukabidhiwa jukumu la kuipeperusha bendera ya chama hicho, ni kumchagua makamu wake ikizingatiwa kuwa, jamii za mlima Kenya na Magharibi ya Kenya zinakimezea mate kiti hicho. Rigathe Gachagua na Musalia Mudavadi wa ANC wanapigiwa upatu wa kiti hicho.