Yaani ukiangalia mazingira ya vyoo katika ofisi au mazingira ya serikali ni kero tupu, achilia mbali vyuo na hospitali.
Siku moja uongozi wa ARUSHA DC walikuja kukagua usafi shule moja Private. Walipokosa cha kuandika, wakazunguka wee baadaye wakasema Karo la kuoshea linaelekeza maji kwenye open space, hivyo tulipe faini. Walitusumbua, na kuandika faini. Siku moja nikafika kwenye ofisi zinazowatuma hao wapiga faini, nilitamani niwaone niwahoji juu ya fedha waliyochukua. Ofisi zao zilikuwa ni JALALA. Kuanzia nje, mapokezi, Vyoo, ilikuwa uchafu kipeo cha pili. Shame on them.