Pre GE2025 Ruvuma: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Ruvuma: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ruvuma.jpg

Mkoa wa Ruvuma. Umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Umepakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki.

Makao makuu ya mkoa yako Songea mjini. Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu
katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,848,794; wanaume 902,298 na wanawake 946,496.

Mkoa huu una Halmashauri nane (8) katika mchanguo wa Mamlaka za Miji na Mamlaka za Wilaya

Mkoa wa Ruvuma una majimbo ya uchaguzi tisa (9) ambapo Jimbo la Songea Mjini linaongoza kwa kuwa na watu wengi (286,285) likifuatiwa na Jimbo la Mbinga Vijijini (watu 285,582). Jimbo lenye idadi ndogo ya watu ni Madaba ambalo lina watu 65,215.

Majimbo ya Uchaguzi

Jimbo la Songea Mjini
(Watu 286,285 ambapo wanaume ni 134,920 na wanawake 151,365)

Jimbo la Madaba (Watu 65,215, ambapo Wanaume ni 33,085 na Wanawake ni 32,130)

Jimbo la Mbinga Vijijini (Watu 285,582, ambapo Wanaume ni 141,271 na Wanawake ni 144,311)

Jimbo la Mbinga Mjini (Watu 158,896, ambapo Wanaume ni 75,882 na Wanawake ni 83,014)

Jimbo la Nyasa (Watu 191,193 , ambapo Wanaume ni 93,494 na Wanawake ni 97,699)

Jimbo la Namtumbo (Watu 271,368, ambapo Wanaume ni 132,035 na Wanawake ni 139,333)

Jimbo la Tunduru Kaskazini (Watu 225,773, ambapo Wanaume ni 110,614 na Wanawake ni 115,159)

Jimbo la Tunduru Kusini (Watu 186,281, ambapo Wanaume ni 91,054 na Wanawake ni 95,227)

Soma Pia:
Hali ya kisiasa
Kama ilivyo kwa mikoa mingine, uchaguzi wa Ruvuma unadhihirisha changamoto za uwakilishi wa kisiasa na ushindani wa kidemokrasia. Katika majimbo yote 9 yalichukuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
katika jimbo la Tunduru Kusini ambako Daimu Mpakate (CCM) alipata kura 26,982 dhidi ya Abdalah Mtutula (ACT-Wazalendo) aliyepata kura 23,968.

Katika jimbo la Madaba, Joseph Kizito Mhagama alipita bila kupingwa. Katika baadhi ya majimbo kama Peramiho na Nyasa, kulikuwa na tofauti kubwa ya kura kati ya wagombea wa CCM na wa upinzani.

Peramiho -
Jenista Mhagama (CCM) - Kura 27,479
Silvester Mapunda (CHADEMA) - Kura 3,440

Nyasa:
Eng. Stella Manyanya (CCM) - Kura 34,937
Casberth Kiwango(CHADEMA) - Kura 4,055.

Katika majimbo kama Songea Mjini na Tunduru Kusini, upinzani ulionekana kufanya vizuri zaidi ikilinganishwa na majimbo mengine, ingawa hawakufanikiwa kushinda.

Dkt. Damas Ndumbaro(CCM) - Kura 39,783
Aden Mayala(CHADEMA) - Kura 15,146

Daimu Mpakate (CCM) - Kura 26,982
Abdalah Mtutula (ACT Wazalendo) - Kura 23,968.

JANUARI
FEBRUARI
MACHI
 
Back
Top Bottom