DOKEZO Ruvuma: Mpango wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Songea una shida, kuna mazingira ya ubababishaji

DOKEZO Ruvuma: Mpango wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Songea una shida, kuna mazingira ya ubababishaji

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Joined
Sep 23, 2024
Posts
64
Reaction score
43
Screenshot_20241202-182820.png


Uamuzi wa Serikali kupeleka Mradi wa Kusaidia Kaya Masikini (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni uamuzi mzuri, wamefanya vizuri kupeleka mpango huo kwenye Halmashauri ila kuna changamoto kubwa kwa wasimamizi wa mfuko wamekuwa na utata sana kwa walengwa wanaopokea pesa kutoka TASAF.

Moja ya changamoto ambayo imekuwa ikitokea ni baadhi ya wahusika kuondoa wanufaika kwenye mfumo kwa vigezo kwamba anajimudu kiuchumi, jambo ambalo halina ukweli.

Pia katika kulitekeleza hilo wamekuwa hawasemi ukweli kwa wanufaika kwa maana hawaambiwi kama wameondolewa kwenye mradi.

Kuna watu ambao ikifika muda wao wa kwenda kuchukua fedha za TASAF hawazipati na ukifika muda wa wao kwenda kuhoji pia hawapewi majibu ya kueleweka.

Viongozi wa ngazi za juu wa TASAF wanapokuja kwenye Halmashauri hii wanaondoka na taarifa kuwa mambo yapo safi, kwasababu hawaonani na Wananchi ili wasikilize kero zao badala yake wanakutana tu na viongozi wetu wachache, wanazungumzia ofisini kisha wanaondoka kwa kujiridhisha na taarifa walizopewa.

Mfano Oktoba 3, 2024 alikuja Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Shadrack Mziray na kuondoka na taarifa ya kutokuwa na malalamiko juu ya wanufaika walioondolewa kwenye mpango, wakati huku nyuma malalamiko ni mengi.

Wanufaika wa fedha hizo baadhi yao hawaelewi kwanini hawapati zaidi ya Mwaka sasa.

Pia, soma; √ - Mkurugenzi Mtendaji wa Songea, Bi Elizabeth Gumbo amesema, TASAF inafika kwenye Vijiji vyote 56 kupokea Malalamiko

Kuna wanufaika ambao hawapewi majibu ya kueleweka wanapouliza ofisi zinazohusika na ugawaji wa pesa hizo kuwa kwanini pesa hawapati, majibu yamekuwa ya ubabaishaji kama vile utatumiwa mpaka mwaka umeisha au kafuatilie mjini (Manispaa).

Wafanyakazi wanasema hayo wakati wanajua kati yao hawawezi kufuatilia na baadhi ya wanaojaribu kwenda wanaambulia patupu.

Safari za nenda rudi huko Manispaa mpaka imefikia hatua Wanufaika wengi wamechoka.

Mfano, Kata ya Peramiho kuna uhuni umefanyika kwa wanufaika kwasababu kuna ambao awali walikuwa wanapokelea Peramiho A, baadaye waligawanywa katika makundi mawili, baadhi wakabaki Peramiho A na wengine majina yao yalihamishiwa Ofisi ya Mtaa wa Nguvu Moja.

Mchakato wa ugawaji huo majina yaliyotolewa Peramiho A kwenda nguvu moja baadhi yao hawajawahi kupata pesa hizo na majina yao yapo ofisini kuwa nao ni wanufaika.

Wakiulizwa wanaambiwa wataingiziwa kwenye simu, lakini hilo halijafanyika zaidi ya mwaka sasa. Kama wameondolewa kwanini wasiwaambie kwamba mmeondolewa na majina yao yafutwe?

Screenshot_20241202-164911.jpg

Screenshot 2024-12-10 111710.png

Wengine waliingizwa kwenye mfumo kwa ajili ya Watoto yatima walioachiwa na ndugu zao cha kushangaza, wameondolewa wakati Watoto hao hawajamaliza hata shule ya msingi na mlezi maisha yake bado ni magumu.

Wakati huohuo, upande wa pili wanatoa taarifa kuwa walioondolewa wanajiweza kiuchumi.

Achilia mbali waliondolewa kwa wale wanaoendelea kupokea unakuta mwezi huu kapata mwezi ujao hakuna kitu kanakuwa kama kautaratibu kwa mwaka miezi kadhaa unarukwa.

Ikiwa mamlaka zinaona tabu kuendeleza mradi huo basi kuwe Na utaratibu mnufaika yoyote apate pesa kwa miaka kadhaa baada ya hapo awe ameinuka kiuchumi au hajainuka basi hasiendelee kupewa sambamba na vitambulisho vyao kuweka tarehe ya
mwisho (expire date).

Pia, viongozi wa juu mnapokuja msiishie ofisini itisheni mikutano ya hadhara na kuruhusu wananchi wazungumze.
 

Attachments

  • Screenshot_20241202-164932.png
    Screenshot_20241202-164932.png
    1 MB · Views: 4
Back
Top Bottom