KERO Ruvuma: Shule ya Msingi Miembeni (Mbinga Mji) hali yake ni mbaya sana, Miundombinu imechoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
​
Shule ya Msingi MIEMBENI ipo Kijiji cha MIEMBENI, Kata ya Kitanda Halmashauri ya Mbinga Mji, hali halisi ni kuwa haishawishi kabisa suala zima la kufundisha wala kujifunzia.

Madarasa hayana madirisha wala milango... Majengo ya madarasa ya shule hii ni kama magofu yaliyosahaulika, Wanafunzi wanapigwa sana na baridi na wakati wa mvua hali inakuwa mbaya zaidi.

Mazingira haya yanasababisha hata Walimu wanaopangwa kufundisha kwenye shule hii na kuishia kuomba uhamisho. Shule hii pia ina Walimu 4 tu ambao wote ni wakiume, hivyo watoto wa kike hawana mlezi wa kuweza kufikisha matatizo yao...... Viongozi husika wa elimu waweze kutatua kero hizi.
​
 
Na hii picha shule ya ghorofa ndio ndoto yao ?
Aisee, kama ndio mimi nikimaliza hio shule, kwanini nisikimblie daslama kutafuta maisha.....

 
Kwa msaada wa watu kutoka Marekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…