Pre GE2025 Ruvuma: Wazee wa Madaba wamuomba Dkt. Joseph Mhagama agombee tena Ubunge 2025

Pre GE2025 Ruvuma: Wazee wa Madaba wamuomba Dkt. Joseph Mhagama agombee tena Ubunge 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Naona wazee wamesha lamba asali na imekolea utamu! Mpaka nao hawana maana wamekalia uchawa! Tunaenda wapi?

Taratibu CCM wanaanza kuingiza mambo za kupita bila kupingwa, tusipokaa vizuri hii itasongea mpaka kwenye uchaguzi Mkuu warudishe mambo mambo za 2020.

Imeanza kwa Samia na Nchimbi, ikaenda kwa Silaa, kwa Mchengerwa nako, huku nako upuuzi unaendelea. Hii sio bahati mbaya wakuu, kuna jambo linakuja.

=====

Wazee wa Jimbo la Madaba, mkoani Ruvuma, wakiongozwa na Chief Yukundusi Chabruma Tawete, wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo, Dkt. Joseph Kizito Mhagama, kugombea tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ili aendelee kuwatumikia wananchi.

Soma Pia:
Tamko hilo limetolewa na Baraza Huru la Wazee baada ya mkutano wao uliofanyika katika Kijiji cha Kipingo, Kata ya Lituta, Halmashauri ya Madaba, Wilaya ya Songea. Wazee wa kimila walioshiriki mkutano huo wamesema wamefikia azimio hilo kutokana na kazi kubwa aliyofanya Mbunge Mhagama katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

 
Looh! Nilijua mhagama yule mama wa wizara ya Afya ningechekaa balaaa!

Tangu lini awe dokta wakati wote tunajua JENISTA ana DIPLOMA ya hapa na pale!!
 
Back
Top Bottom